MWENYEKITI UWT KIBAHA KWA KUSHIRIKIANA NA BENKI YA AZANIA WATOA MAFUNZO KWA WAJASILIAMALI KATA YA MISUGUSUGU

Na Gustaphu Haule, Pwani
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi ( UWT) Kibaha Mjini Elina Mgonja kwa kushirikiana na Benki ya Azania wameweka kambi ya siku moja katika Kata ya Misugusugu kwa ajili kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa Wanawake wa Kata hiyo.
Mgonja na maafisa wa Azania Benki wameweka kambi hiyo Agosti 10,2026 katika viwanja vya mpira wa miguu Misugusugu ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara ya kutoa mafunzo hayo katika Kata mbalimbali za Kibaha Mjini.
Akiwa katika Kata ya Misugusugu Mgonja amekutana na Wanawake wa kutoka Tawi la Vitendo,Miomboni, Saeni,Jonuga,Zogowale,Karabaka Juu na Karabaka Bondeni na kuwafundisha kutengeneza vitenge vya Batiki, Sabuni za aina mbalimbali na mafuta ya ngozi.
Mwenyekiti wa UWT Kibaha Mjini Elina Mgonja ( aliyekaa kwenye kiti) akiwafundisha Wanawake wa Kata ya Misugusugu kutengeneza Sabuni Agosti 10,2026.Akizungumza katika mafunzo hayo Mgonja amesema kuwa amelazimika kushirikiana na Benki ya Azania ili kusudi mara baada ya mafunzo hayo Wanawake waweze kupata mikopo ambayo itakuwa mitaji katika kuanzisha na kuendeleza shughuli zao za kijasiriamali.
Mgonja,amesema yeye anapita kufundisha ujasiriamali lakini ameona sio vyema Wanawake hao wakabaki wakihangaika kutafuta mitaji na badala yake watumie fursa ya mikopo kutoka Benki ya Azania ili waendeleze shughuli zao za kijasiriamali.
Mgonja amesema lengo lake kubwa ni kuwakwamua kiuchumi Wanawake wa Kibaha Mjini kupitia shughuli za kijasiriamali ili waweze kujitegemea katika maisha yao na familia zao.
Mwenyekiti wa UWT Kibaha Mjini Elina Mgonja akizungumza katika mafunzo ya ujasiriamali kwa Wanawake wa Kata ya Misugusugu yaliyofanyika Agosti 10,2026."Leo nimekuja na maafisa kutoka Benki ya Azania kwakuwa nimeona wanafursa nzuri ambayo Wanawake wakiitumia wataweza kupata mafanikio makubwa hapo baadae kwani nataka kuwaona Wanawake wa Kibaha kila mmoja anajishughulisha na masuala ya kujenga uchumi",amesema Mgonja.
Meneja Mahusiano wa Azania Benki tawi la Kibaha Happiness Lema, amesema anamshukuru mwenyekiti wa UWT Kibaha Mjini kwa kukubali kuungananae katika ziara hiyo kwani lengo la Azania Benki ni kuwafikia Wanawake wote wa Kibaha Mjini.
Meneja Mahusiano wa Azania Bank tawi la Kibaha Happiness Lema akizungumza na Wanawake wa Kata ya Misugusugu Agosti 10,2026.Amesema Azania Benki inatoa kipaumbele kwa Wanawake katika kuwakwamua kiuchumi na ndio maana imekuja na akaunti maalum ya Wanawake inayoitwa Mwanamke Hodari.
Maafisa wa Azania Bank wakitoa huduma kwa Wanawake wa Kata ya Misugusugu katika mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa Agosti 10 2026 na Mwenyekiti wa UWT Elina Mgonja.Amesema Mwanamke yeyote mjasiriamali anaweza kupata mikopo katika Benki hiyo kuanzia Sh.200,000 hadi Sh.milioni 500 kutegemeana na mzunguko anaohufanya katika akauti yake katika Benki hiyo.
Amesema Mwanamke anaweza kujiwekea fedha katika akaunti yake kidogo kidogo angalau ndani ya miezi sita na wataangalia miamala inavyoingia na kisha kutoka kwenda kutembelea biashara yake ili kuangalia kama amefikia kigezo cha kupata mkopo.
Wanawake wa Kata ya Misugusugu wakiwa katika mafunzo ya ujasiriamali yaliyokuwa yakitolewa na mwenyekiti wa UWT Kibaha Mjini Elina Mgonja Agosti 10,2026."Lengo la kuambatana na Mwenyekiti wa UWT katika ziara hii ya mafunzo ya ujasiriamali ni kuwajulisha kuwa Benki ya Azania sasa ipo Kibaha na imekuja na akaunti maalum ya Wanawake inayoitwa "Mwanamke Hodari " furaha yetu ni kuona mnapata mafunzo na mnajua wapi mnaenda kupata mikopo kwa ajili kuanzisha na kuendeleza shughuli zenu,"amesema Lema.
Wanawake wa Kata ya Misugusugu wakifurahia katika mafunzo ya ujasiriamali baada ya Mwenyekiti wa UWT kutengeneza Kitenge cha Batiki kama kinavyoonekana pichani.Lema amewaomba Wanawake wa Kibaha Mjini kuhakikisha wanatumia vyema fursa iliyopo katika Benki hiyo ili iweze kuwasaidia kupata mikopo ya uhakika na hivyo kuweza kuendeleza shughuli zao za kijasiriamali kwa urahisi zaidi.
Diwani wa Kata ya Misugusugu Ally Simba amemshukuru mwenyekiti wa UWT Kibaha Mjini Elina Mgonja kwa kuona umuhimu wa kuwafundisha Wanawake wa Kata yake masuala ya ujasiriamali.
"Nimefurahi kuona mnapata mafunzo ya ujasiriamali kutoka kwa Mwenyekiti wa UWT lakini nafurahia pia kuona Benki ya Azania imetufikia katika Kata yetu ,hakika ni jambo la kujivunia na mimi sitowaacha nyuma kwani tutashirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha mafunzo haya yanaleta manufaa,"amesema Simba.
Simba amesema kuwa kupata mafunzo hayo ni mwanzo wa kupiga hatua ya kusongambele katika kujikwamua kiuchumi ambapo amesema ni vyema wazingatie mafunzo hayo kwa umakini na ikiwezekana wawe walimu kwa Wanawake wenzao ambao hawakubahatika kushiriki mafunzo hayo.





Post a Comment