DC MASWA AKABIDHI PIKIPIKI KWA WATOA HUDUMA YA MAJI NGAZI YA JAMII
Na Samwel Mwanga, Maswa
MKUU wa wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu, Aswege Kaminyoge amekabidhi pikipiki mbili aina ya TVS kwenye Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSO) za Shishiyu na Njiapanda zilizoko wilayani humo ili kurahisisha kutoa huduma kwenye maeneo ya vijiji wanavyovihudumia.
Pikipiki hizo zimenunuliwa na Mkandarasi Afrihost Investment Ltd aliyekuwa akitekeleza ujenzi wa Mradi wa Maji Malekano-Kadoto wilayani humo ikiwa ni sehemu ya kutekeleza kipengere cha ununuzi wa pikipiki mbili zenye thamani ya Tsh. Milioni saba chini ya Mradi wa Lipa kwa Matokeo(Pfor R)ambao ni Program ya Maji chini ya Mkopo wa Benki ya Dunia.
Akikabidhi pikipiki hizo kwenye viwanja wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dc Kaminyoge amesema huduma ya upatikanaji wa maji katika wilaya ya Maswa imegawanyika katika maeneo mawili ya mjini na vijijini kwa lengo la kumtua mama ndoo kichwani.
Mkuu wa wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyoge(mwenye miwani)akimkabidhi pikipiki Mwenyekiti wa CBWSO Njiapanda,Mbuga Ubaya(kulia) katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Maswa.
Amesema kuwa kwa upande wa vijijini, Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(Ruwasa)wamefanya kazi kubwa ya kuhakikisha wananchi wanapata maji kupitia miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu ambaye amekuwa akileta fedha katika kutekeleza miradi hiyo iliyoko wilayani humo.
Amesema lengo la kukabidhi pikipiki hizo ni kurahisisha kufika kwenye eneo lenye changamoto ya maji kwa haraka na kuitatua ukizingatia kila jumuiya ina eneo kubwa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi katika vijiji vyao na zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
Pikipiki mbili zilizotolewa na Ruwasa wilaya ya Maswa kwa Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji ngazi ya jamii(CBWSO)za Shishiyu na Njiapanda .
“Nimarufuku kutumia pikipiki hizi kama bodaboda ukibainika tutakushughulikia kwani RUWASA wilaya ya Maswa imenunua kwa lengo la kuhakikisha unafika kwa wakati eneo lenye changamoto ya kutotoa maji”,amesema.
Pia amwasihi kuzitunza ili zidumu kwa muda mrefu na kuhakikisha kuwa lengo la serikali linafikiwa la utoaji wa huduma ya maji kwa maeneo ya vijijini inafikia asiliamia 85 hadi kufikia mwaka 2025 kama ilivyoelezwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)ya mwaka 2020 hadi 2025.
Baadhi ya watumishi wa serikali katika wilaya ya Maswa waliojitokeza katika Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Maswa kushuhudia kukabidhiwa kwa pikipiki kwa CBWSO za Shishiyu na Njiapanda
Aidha amesema kuwa Ruwasa iendelee kuvisaidia Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji ngazi ya jamii kwa kuwa vilivyo vingi bado havina uwezo wa kujitegemea kutokana na kutokuwa na fedha za kutosha kwa ajili ya kujiendesha sambamba na kutoa elimu katika miradi ya maji hasa katika suala la uendeshaji.
Naye Mbunge wa jimbo la Maswa Magharibi, Mashimba Ndaki amesema kuwa pamoja na Ruwasa kufanya kazi kubwa sana ya upatikanaji wa maji katika wilaya ya Maswa hususan katika jimbo lake ambalo kati ya Kata 17 ni Kata 3 ndizo hazina maji titirika kwa baadhi ya vijiji lakini ina changamoto ya vitendea kazi kama vile pikipiki na magari.
Mbunge wa jimbo la Maswa Magharibi, Mashimba Ndaki(kushoto)akizungumza katika hafla ya kukabidhi pikipiki kwa CBWSO ya Shishiyu na Njiapanda.
“Ruwasa mnafanya kazi nzuri sana hasa katika jimbo langu la Maswa Magharibi ni kama vile mmenipendelea maana katika Kata 17 ni Kata 3 tu ambazo hazina maji tiririka katika baadhi ya vijiji ila bado mnakabiliwa na upungufu wa vitendea kazi kama vile pikipiki na magari ,”
“Hivi vyombo vya watoa huduma ngazi ya jamii vyote vinahitaji kuwa na vyombo vya usafiri kama pikipiki ili kuwarahisishia kufika kwa haraka kwenye eneo lenye changamoto na kuitatua hata Ruwasa makao makuu ya wilaya gari lao ni bovu hivyo niiombe serikali iweze kuwapatia gari nyingine wawweze kutekeleza majukumu yao kwani wilaya hiyo ni kubwa ina vijiji 120,”amesema.
Awali Afisa Maendeleo Ruwasa wilaya ya Maswa,Wilson Magaigwa amesema kuwa vyombo hivyo vya watumiaji Maji ngazi ya jamii(CBWSOs) vimekuwa vikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya uhaba wa vyombo vya usafiri kwani maeneo ya utekelezaji ni makubwa sana.
“CBWSOs moja katika wilaya ya Maswa inaweza kuhudumia zaidi ya kijiji kimoja huku akitolea mfano kwa CBWSOs za Njiapanda ina vijiji viwili na Shishiyu ina vijiji sita hivyo kusababisha wakati mwingine utendaji wa Vyombo hivyo kushuka,”amesema.
Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa wilaya ya Maswa,Mhandisi Lucas Madaha amesema kuwa kwa kipindi cha miaka Miwili ya Uongozi wa Rais Dkt Samia Sukuhu wilaya hiyo wameweza kuongeza upatikanaji wa maji vijijini kutoka Ailimia 68.9 kwa mwaka 2019 na kwa sasa wamefikia asilimia 74.6.
Meneja wa Ruwasa wilaya ya Maswa, MhandisiLucas Madaha(kulia)akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyoge(aliye kati)wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki kwa CBWSO ya Shishiyu na Njiapanda.
Mwenyekiti wa CBWSO Njiapanda, Mbuga Ubaya ambaye amepatiwa pikipiki kwa ajili ya kuhudumia eneo lake lenye vijiji vya Njiapanda na Isanga.
Mkuu wa wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyoge(mwenye miwani)akimkabidhi pikipiki Mwenyekiti wa CBWSO Njiapanda,Mbuga Ubaya(kulia) katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Maswa.
amesema kuwa ataitumia pikipiki hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuondoa changamoto zinazowakabili wananchi wanaotumia maji katika eneo hilo ambalo analihudumia.
Naye Msimamizi wa CBWSO ya Shishiyu,Stephen Fabian amemwahidi mkuu wa wilaya kuitumia pikipiki hiyo kwa lengo lililohitajika hivyo kuwahaidi wananchi kutoa taarifa ya changamoto pindi inapotokea kwenye vijiji vya Shishiyu,Mwaliga,Kakola, Malekano na Mwanganda ili afike kwa wakati kutatua.
Post a Comment