TASOA YAPOKEA MSAADA
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Michezo Tanzania (TASOA), Benson Maneno amepokea msaada wa awali wa T-shirt 50 kutoka Kampuni ya Ace Diamond kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Maafisa Michezo Tanzania.
Amepokea msaada huo, tarehe 11, Machi, 2026 jijini Arusha. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika jijini Arusha katika Ukumbi wa AICC, ukihusisha maafisa michezo kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Akipokea msaada huo, Maneno ameishukuru Kampuni ya Ace Diamond kwa ushirikiano na mchango wao katika kusaidia maandalizi ya mkutano utakaofanyika Tarehe 28-30 . Muhimu kwa maendeleo ya sekta ya michezo nchini.

Post a Comment