HEADER AD

HEADER AD

MNKONDYA AFUNGUA FURSA ZAO LA VANILLA NCHINI KENYA

Na Mwandishi Wetu, Kenya 

KAMPUNI ya Vanilla Internation imefungua fursa kwa kuanzisha mradi mpya wa Vanilla Village Kenya katika mji mdogo wa Mariakani, Mombasa.

Awali akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi wa Vanilla International Limited Duniani, Simon Mnkondya amesema amechukuwa uamuzi huo baada ya kuona Wananchi wa Kenya wengi wanachangamkia katika kilimo cha Vanilla kama fursa za ajira na uchumi zaidi.


"Ni wakati sahihi kwa Kenya kuanza kilimo cha Vanilla kwa mfumo wa mashamba Shufwaa (block farming) ili kupunguza gharama za uwekezaji, kwa ajili ya usalama na kwa ajili ya kuhakikisha uwepo wa soko la Vanilla.

Aidha, Mnkondya ameongeza kuwa, Vanilla International Limited itafanya mradi ikishirikiana na Taasisi ya MRM Foundation na KARIBUNI Foundation zote za Kenya na Taasisi ya Society Watch ya Tanzania. 

"Lengo la mradi wa Vanilla Village Kenya ni kukuza uchumi wa Wakenya na Waafrika kwa ujumla kwa sababu bei ya vanilla imewahi kufikia mpaka Dola za Kimarekani 500$ takribani 1,000,000/= ya kitanzania. 

"Wadau wanaweza kuwasiliana nasi kupitia mitandao yetu ya kijamii ama  kufika ofisi zetu zilizopo Dar es Salaam,  Arusha." Amesema Mnkondya.

Kwa upande wao baadhi ya washirika katika mradi huo, akiwemo Dipan Shah Mkurugenzi wa Nyali Cinemax amesema Vanilla India imewafanya wakulima wawe matajiri sana kwa maana ni zao la pili kwa bei duniani.


Nae Bruno Cern'o  Raisi wa Upendo Foundation mwenye Asili ya Italia amesema kwa vile Vanilla ni zao la bei kubwa ni vyema sasa Waafrika kulima Vanilla ili kupata utajiri endelevu na kuwa na unafuu wa maisha.

Gianfranco Ranieri ambaye ni Raisi wa Karibuni Assogiocattoli ya Milano Italia ameahidi kulima heka zaidi ya 100 hapa Kenya na anaenda kulima zao hilo kwa nguvu zote.


Nae Siprosa Rabach ambaye ni Meneja mkazi wa MRM Foundation amesema zao hilo litasaidia Kenya watu kupata kazi na kipato.

Mnkondya kupitia zao hilo la Vanilla, pia anaendesha miradi mbalimbali ikiwemo Vanilla Village Arusha, Vanilla Village Dubai,  Vanilla Village Dodoma, Vanilla Village Zanzibar na mengine mengi.

No comments