HEADER AD

HEADER AD

MWANA MWAMSINGIZIA

VIBAYA wanamsema, dada yetu Mariamu,
Hata hawana huruma, tabia zao ni ngumu,
Wameshindwa kusimama, wameanza kuhujumu,
Kosa katenda mwingine Mwana mwamsingizia.

Sumu acheni kutia, Mwana kumsingizia,
Napenda kuwahusia, acheni kutia doa,
Wivu unawasumbua, mengi kuyasingizia,
Kosa katenda mwingine Mwana mwamsingizia.

Makosa hana hakika, msimtoe imani,
Acheni kuhangaika, na dhambi jiepusheni
Ipo siku mtachoka, nayasema si utani,
Kosa katenda mwingine Mwana mwamsingizia.

Chuki zenu ni za nini, kipi amewakosea
Siyo dhambi kugombea,  nawe waweza gombea,
Najua anagombea, ndiyo mana mwachukia,
Kosa katenda mwingine Mwana mwamsingizia.

Tuache chuki jamani, tupendane kwa imani,
Kwa Mungu ni mtihani, panatisha kaburini,
Tuwe ni wenye imani, ya wengine kuthamini,
Kosa katenda mwingine Mwana mwamsingizia.

Baba yake mhusika, ya Mwana hapa ya nini ?
Namaliza kuandika, nina uchungu moyoni,
Huzuni imenifika, Kuna mambo duniani
Kosa katenda mwingine Mwana mwamsingizia.

Mtunzi ni SirDody- Kilimanjaro
0675654955 au 0762396923

No comments