HEADER AD

HEADER AD

WARAKA: BENDERA YA TAIFA ITUNDIKWE KWEYE MAJENGO YA SERIKALI, TAASISI

Na Dinna Maningo, Tarime

UONGOZI wa shule ya Sekondari Bukenye Kata ya Manga, Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara umeweka Bendera ya Taifa na Kibao cha shule katika shule hiyo ambapo awali havikuwepo.

Januari, 2, 2023, DIMA Online iliripoti habari kuhusu changamoto za shule hiyo ikiwemo ya kutotundikwa Bendera ya Taifa na Kibao kutokuwekwa tangu ianzishwe mwaka 2021.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Manga Samwel Mseti aliyefika kwenye shule hiyo kufahamu changamoto za shule alisema kwamba katika utoaji wa elimu bora Ilani ya CCM inatakiwa kutekelezwa katika shule hiyo, nakuahidi kusimamia kuhakikisha changamoto za shule zinatafutiwa ufumbuzi.

                Mwenyekiti CCM Manga

"Tumechaguliwa hivi karibuni na bahati nzuri nimefanya ziara ya kushtukiza hapa shuleni nikakuta ina changamoto nyingi haina kibao cha shule, hakuna Bendera ya Taifa, madarasa ni pungufu na hakuna viti na meza kwa baadhi ya madarasa , lazima Ilani itekelezwe na lazima tumuunge rais kwa vitendo" amesema Samwel. 

Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vanance Babukege alipoulizwa sababu ya shule hiyo kutokuwa na Bendera na Kibao alisema.

" Bukenye haina Bendera!! ngoja niwasiliane na mkuu wa shule. Suala la bendera na kibao cha shule vinatakiwa kuwekwa na mkuu wa shule" alisema Vanance.

             Kibao cha Shule kilichowekwa hivi karibuni.

    Waraka wa Utumishi

Kumekuwepo na kupuuzwa kwa utundikaji wa Bendera ya Taifa katika majengo ya Serikali na Taasisi zake jambo ambalo ni kinyume na waraka wa Utumishi Na. 2 wa mwaka 2000 wa utundikaji na upepetushaji wa Bendera ya Taifa, Bendera ya Rais na Picha za Viongozi.

Katika upandishaji wa Bendera ya Taifa na upepetushaji waraka huo umeelekeza taratibu za utundikaji na upepetushaji ikiwa ni pamoja Bendera hiyo ya Taifa kutundikwa kwenye majengo yote ya serikali na taasisi zake, ikiwa ni pamoja na serikali za mitaa.

      Bendera ya Taifa shule ya Sekondari Bukenye iliyowekwa hivi karibuni.

Pia Bendera ya Taifa itapepea mahali pengine penye shughuli za Serikali ambazo zitahudhuriwa na viongozi wa ngazi za ya juu ya Taifa, Mkoa na Wilaya.

Bendera zitakazo pepezwa katika sehemu hizi itabidi ziondolewe mara baada ya shughuli hizo kumalizika.

Waraka umeeleza kuwa Wakuu wa Wilaya na Watendaji Wakuu wanaoteuliwa na Rais watapepeza Bendera ndogo ya Taifa kwenye meza ofisini mwao; na hawatapepeza bendera kwenye magari yao.

         Bendera ya Taifa 

Pia Bendera ya Taifa itapepea kwenye makazi rasmi ya viongozi.Viongozi watakaopepeza Bendera kwenye makazi yao ni Rais,Makamu wa Rais,Waziri Mkuu,Spika,Jaji Mkuu,Mawaziri na Naibu Mawaziri,Wakuu wa Mikoa na Wilaya.

Waraka unasema Bendera ya Taifa haitapepezwa kwenye makazi binafsi ya viongozi hawa. 

Wakuu wa Mikoa watapepeza Bendera katika Mikoa yao. Bendera ya Taifa itapepea upande wa kushoto wa gari.

Hata hivyo Wakuu wa Mikoa awatapepeza Bendera ya Taifa mahali popote alipo Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.


Bendera ya Taifa ya Tanzania

No comments