JESHI LA POLISI LAWASHIKILIA 17 KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI
Na Alodia Babara, Kagera
JESHI la polisi mkoani Kagera linawashikilia watu 17 kwa ajili ya mahojiano kwa tuhuma za uchochezi mitandaoni pamoja na kuchana mabango ya wagombea.
Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Kagera Blassius Chatanda ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema kuwa, miongoni mwa waliokamatwa ni pamoja na wanaohamasisha watu kuandamana siku ya uchaguzi Oktoba, 29, 2025.
Chatanda ameeleza kuwa, jeshi hilo linao askari wa kutosha kila kanda, kata hadi kituo na wanayo magari ya kutosha kwa ajili ya kufanya doria hivyo wasiwepo watu wa kuandamana wala wanaojifanya wanalinda kura.
"Ulinzi wa kura ni jukumu la polisi sio mwananchi wale wanataka kufanya sisi jeshi la polisi tupo kazini , mpiga kura akikamilisha atoke na aende kupumzika adumishe ustaarabu"amesema Chatanda.
Amesema, kwa wale watakaojifanya kuandamana na kusababisha vurugu siku ya uchaguzi Oktoba 29 mwaka huu jeshi hilo litafanya doria maeneo yote kwa wale wanaojiandaa kufanya hivyo wasidhubutu.


Post a Comment