KADA WA CCM AJIUA NA KUACHA UJUMBE AKITAKA MPENZI WAKE ASAKWE
>> Atoa namba yake ya siri ya simu na ya mpenzi wake akitaka atafutwe
DIMA Online, Tarime
KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wambura Kisike maarufu kwa jina la Macheda, mkazi wa Kata ya Nyamisangura mtaa wa msati ,wilaya ya Tarime mkoani Mara, ambaye umri wake haujafahamika amekutwa amejinyonga kwa shuka chumbani kwake.
Marehemu anadaiwa kujinyonga chumbani kwake nyumbani kisha kuacha barua yenye ujumbe wa maneno huku akimtaja mwanamke mmoja kwa jina la Eva kwamba yeye ndio sababu ya kujinyonga.
Katika barua hiyo ameandika namba za simu akiomba Eva atafutwe kwamba amezaa nae mtoto.
Barua hiyo ambayo haijathibitika kama kaiandika yeye ama la inasema hivi " Nimefanya hivi kwasababu ya Eva amenitesa sana namchukia sana . Familia yangu ,rafiki zangu nimewakosea sana .
" Password ( namba za Siri) yangu ya simu ni 2000, mtafuteni Eva kwa simu ........ana mtoto wangu" imeeleza barua hiyo.
Barua hiyo na namba za Eva tumezihifadhi.


Post a Comment