HEADER AD

HEADER AD

MAJINA YA WALIOCHUKUA FOMU NA KUREJESHA WAKIWANIA UBUNGE TARIME MJINI, VIJIJINI


>> Katibu CCM Hamza Kyeibanja amesema zoezi limefanyika kwa uhuru na amani

Na Dinna Maningo, Tarime 

JUMLA ya watiania 28  kati yao wanaume 24 na wanawake wanne wamejitokeza kuchukua na kurejesha fomu kwa ajili ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge katika Jimbo la Tarime mjini na Jimbo la Tarime vijijini katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake, Katibu wa Chama cha Mapinduzi ( CCM), wilaya ya Tarime, Hamza Adamu Kyeibanja,  amesema kuwa zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu lilianza Juni, 28, 2025 na kukamilika julai 2, 2025 na kwamba wote waliochukua fomu wamerejesha.

         Katibu wa Chama cha Mapinduzi ( CCM), wilaya ya Tarime, Hamza Adamu Kyeibanja akizungumza.

Amesema jimbo la Tarime mjini waliochukua fomu na kurejesha ni 14 kati yao wanaume ni 12 , wanawake wawili ambao ni Robert Mkirya Chacha mwenye umri wa miaka ( 61) , Gregory Mogendi Nyanchini (85), Cheche Andrew (53), Deodatus Meck Mbaki ( 42), Jackson Ryoba Kangoye ( 38), Samwel Kiboye Namba tatu (56), Musa Ryoba Deus ( 30).

Wengine ni Said Kisyery Chambili (35), Janeth Anthony Mtiba (30) , Magwi Nyang'ombe Itembe (33), Michael Mwita Kembaki (46), Godfrey George Ng'ariba (39) Manchare Heche Suguta ( 46) na Esther Nicholas Matiko (48).

Katika Jimbo la Tarime vijijini waliochukua fomu na kurejesha ni 14 kati yao wanaume 12, wanawake wawili ambao ni Edward Mgelea Machage ( 47), Elizabeth Msabi (46), Nyerere J. Mwera ( 42), Abdullah Amani Chogo (76) , Deodatus N. Waikama (63).

Wengine ni Michael Joseph Ngogo ( 31) , Nyambari Chacha Nyangwine (49), Simon K. Chacha (55), Nicolaus M.Mgaya (42), David Marwa Mokami, Paul Marwa Motega, Mwita Mwikwabe Waitara (49), Rosemary Joseph Ikwabe (38) na John Kengere Bogomba ( 50).

" Majimbo yote waliochukua fomu wamerejesha , hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza kwasababu chama kilikuwa kimeweka taratibu zake.

" Fomu kwa nafasi ya ubunge ilikuwa Tsh. 500,000 kwa nafasi ya udiwani Tsh. 50,000 na fedha hizo zilitumwa kwenye namba ya malipo na meseji zilikuwa zinawafikia wahusika waliolipa fedha ya kuchukulia fomu " amesema Katibu.

Amesema katika Jimbo la Tarime mjini wapiga kura wa chama cha Mapinduzi zaidi ya 2,000 watapiga kura za maoni za kumchagua mgombea ubunge atakayeipeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu ambapo katika Jimbo la Tarime vijijini wapiga kura ni zaidi ya 10,000.

Ameongeza kuwa zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu limefanyika kwa uhuru na amani na kwamba zoezi linalofuata ni vikao vya mchujo huku akiwasisitiza wanachama kuendelea kudumisha amani.

Amepiga marufuku wanachama kufanya vikao visivyo rasmi na kwamba vikao vinavyoendelea ni vile vya kikatiba na kwa wale watakaofanya vikao visivyo rasmi watachukuliwa hatua.

Amewaomba Waandishi wa habari kuungana na chama hicho hatua kwa hatua kwamba endapo wakiona kuna dosari huko mitaani na vijijini  katika kipindi hiki cha uchaguzi wawajulishe viongozi wa chama hicho.

Kwa mujibu wa ratiba ya chama cha Mapinduzi ( CCM), tarehe ya kuchukua na kurejesha fomu ni kuanzia tarehe 28/06/2025  mpaka tarehe 02/07/2025.

Kuteua majina matatu (03) ya wagombea ubunge na udiwani wa Kata ni tarehe 09/07/2025 mpaka tarehe  19/07/2025.

Kujitambulisha kwa wagombea ubunge  wa majimbo kwenye Kata na wagombea udiwani kata ni kuanzia tarehe 27/07/2025 mpaka tarehe 01/08/2025.

Zoezi la kupiga kura za maoni ndani ya chama ni tarehe 02/08/2025 kwa wagombea udiwani wa kata na ubunge wa majimbo kwenye kata. 

Uteuzi wa wagombea (mmoja mpeperusha bendera wa chama) Udiwani wa kata  ni tarehe 11/08/2025. 

Uteuzi wagombea (mmoja-mpeperusha bendera wa chama) Ubunge kila jimbo ni tarehe 20/08/2025 ambao ndio watakaogombea kuchuana na wagombea wengine wa vyama vya upinzani ili kupigiwa kura na wananchi katika uchaguzi mkuu, utakaosimamiwa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi ( INEC ) utakaofanyika mwaka huu.

>>Rejea

Idadi ya waliochukua fomu yapungua

Hata hivyo idadi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi waliochukua fomu mwaka huu wa uchaguzi wa 2025  imepungua ikilinganishwa na mwaka 2020.

Waliochukua fomu mwaka 2020 walikuwa wanachama 56 wakitia nia ubunge katika Jimbo la Tarime mjini na vijijini na katika yao wanachama 53 walirudisha fomu na wanachama watatu hawakurudisha fomu.

Jimbo la Tarime mjini  wanachama 26 walichukua fomu kati yao wanachama 23 walirudisha fomu, wanachama watatu hawakurudisha fomu huku Jimbo la Tarime vijijini wanachama 30  walichukua fomu na wote walirudisha fomu.

Waliotia nia ya ubunge Tarime mjini mwaka 2020 ni Suzy Chambili, Monica Anic­et, Dr.Veronica Robert, Hezbon Mwera, Jackson Ryo­ba, Dr.Edward Machag­e,Julius Mtatiro, Eng­.William Machage,Che­che Andrew,Julius La­baran, Samwel Marwa,E­vangel Otieno.

Wengine ni Michael Kembaki, Jeremia Seba,Gerald Martine,M­wita Joseph, Zakayo Wangwe, Manchare He­che Siguta,Mwita James, Ditu Manko,Philip Nyirabu,Robert Mwitango,Justin Mugendi,Deogratius Meck, Segere Shadrack na Col.Kichonge Masero na miongoni mwao watatu hawakurudisha fomu. 

Kwa jimbo la Tarime vijijini  waliochukua fomu ni aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Mwita Waitara, Joyce Ryoba,Dr.Stella Faustine, Joseph Nyahende,Yusuph Wambu­ra,Chacha Masero,John Gimunta,Mwita Jacob Marwa,Wambura Sagi­re,Thomas Chacha Mwi­ta, Musa Raphael, Ny­erere Mwera.

Wengine ni Nyamhanga David, Dr.Abdalah Chogo, Dr.Paul Mwikwab­e,Mordikae Moset, Eli­akimu Maswi, Nicodemas Keraryo, James Bwir­e, Peter Amos Bhusene, Frank Mniko, Lucas Magoti,Samwel Mantarya, Ngocho Darius, Pius Mawa, Harun Kihengu, Maseke Muhono na Dr.Edward Machage na wote wamerudisha fomu.

Kati ya watiania kwa mwaka 2020, Michael Kembaki aliipeperusha bendera ya CCM na kuwa mbunge wa Jimbo la Tarime mjini huku Jimbo la Tarime vijijini kati ya watiania hao Mwita Mwikwabe Waitara aliipeperusha bendera .

 

No comments