HEADER AD

HEADER AD

KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA SERIKALI UJENZI WA BARABARA


Na Mwandishi wetu,  Ngorongoro

KAMATI ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imefanya ziara ya kukagua miundombinu ya barabara  ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro na kuipongeza Serikali kwa uamuzi wa kujenga barabara ya kutoka geti la Seneto hadi Kreta ya Ngorongoro yenye urefu wa Kilomita 4.2

Mwenyekiti wa kamati hiyo Timotheo Mzava ameeleza kamati yake imefarijika na uamuzi wa kujenga barabara hiyo na kuipongeza Serikali kwa kutoa fedha ya ujenzi huo.

"Tunaipongeza Wizara na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kusimamia vizuri ujenzi wa barabara hii, miaka ya nyuma tuliotembelea huku ilikuwa ni shida kubwa kwa watalii lakini baada kukamilika tumeshuhudia ubora wa  huduma kwa wageni wanaoelekea bonde la Kreta umeimarika na malalamiko yamepungua" amefafanua Mzava.

Mzavaameishauri Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kuendelea  kuboresha barabara zote za kuingia ndani ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ili ziwe bora na kuendelea kupitika kwa muda wote.

‘’Kwa kuwa teknolojia hii ni nzuri na rafiki kwa mazingira hasa kwa maeneo ya Hifadhi kamati inashauri  teknolojia hii iendelee kutumika maeneo mengine yenye hifadhi ndani ya nchi yetu.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja aliyeongozana na Kamati hiyo ameeleza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza ushauri wa kamati ya Bunge kuboresha miundombinu ya barabara hasa za mawe ambazo ujenzi wake ni nafuu kulinganisha na barabara ya lami.

"Barabara hii ina urefu wa Km 4.2, bajeti yake ilikuwa TZS 1.9  Billioni lakini tukajenga kwa TZS 1.7 billioni na kuokoa TZS 200 Millioni, tutaendelea kutumia teknolojia hii katika maeneo yetu ya hifadhi hasa yenye barabara korofi" 

Amebainisha kuwa Wizara inaendelea kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za ujenzi wa miundombinu ambayo ni sehemu mkakati wa kufikia  watalii Milioni 5 mwaka 2025 na kuongeza fedha za kigeni kutoka asilimia 17.5 hadi zaidi ya 30 kwa miaka ijayo.

No comments