HEADER AD

HEADER AD

KANUNI YA ADHABU KUMUINGILIA MTU KINYUME NA MAUMBILE

>> Mtu yeyote ambaye anamruhusu mwanaume kumuingilia yeye mwanaume au mwanamke kinyume na maumbile atakuwa ametenda kosa

Na DIMA Online

KULAWITI ni kitendo cha Binadamu kumuingilia kinyume na maumbile binadamu mwenzake awe jinsia ya kiume ama ya kike, kwa kutaka mwenyewe au kutokutaka mwenyewe.

Sheria ya Kanuni ya adhabu 

Kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 154 (1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16, kinasema kwamba, mtu yeyote ambaye (a) anamuingilia mtu yeyote kinyume na maumbile au, (b) anamuingilia mnyama kimwili au (c) anamruhusu mwanaume kumwingilia yeye mwanaume au mwanamke kinyume na maumbile atakuwa ametenda kosa, na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha na wakati mwingine kifungo kisichopungua miaka thelathini.

Kifungu kidogo cha (2)  kinasema, ikiwa kosa limetendwa chini ya kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki dhidi ya mtoto chini ya miaka kumi, mkosaji atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha.


Kifungu cha 155 kinasema, mtu yeyote ambaye atajaribu kutenda kosa mojawapo katika makosa yaliyotajwa katika kifungu cha 154 atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atawajibika kwa adhabu ya kifungo kisichozidi miaka 20.

>>Rejea

Msisitizo wa Waziri Mkuu

Aprili, 13, 2023 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Kassim Majaliwa wakati akihitimisha hoja zilizotolewa na wabunge bungeni Dodoma, wakati wakijadili mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri mkuu na ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024 alisisitiza suala la kuzngatia sheria za nchi.

Waziri Majaliwa alisema sheria za Tanzania zinakataza bayana vitendo vinavyokinzana na utamaduni, mila na desturi, na zimewekwa adhabu mbalimbali kwa makosa ya namna hiyo na yale ya udhalilishaji kwa watoto ikiwemo ulawiti.

    Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Waziri mkuu alizitaka wizara za kisekta kusimamia kikamilifu sheria, kanuni na miongozo iliyopo pamoja na kuchukua hatua za kisheria kwa wote watakaobainika kufanya vitendo kinyume na maadili ya Taifa.

"Uwepo wa matukio yanayokinzana na utamaduni, mila, desturi za kitanzania umehatarisha uimara na ustawi wa jamii na mustakabali wa Taifa kwa ujumla." alisema Waziri Mkuu.

Pia alizisisitiza Asasi za kiraia kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa vibali vyao na usajili " Kwa taasisi zitakazobainika kwenda kinyume na malengo ya usajili ikiwemo kuhamasisha mmomonyoko wa maadili na vitendo vinavyokinzana na mila, tamaduni na desturi, zitachukuliwa hatua za kisheria " alisema".

Aliwaomba viongozi wa dini kuendelea kuwakumbusha waumini wao kuzingatia maadili mema.

Ikumbukwe kuwa anaehusika kutoa ushahidi wa kulawitiwa ni yule aliyefanyiwa kitendo hicho cha kunajisiwa kinyume na maumbile, kisha vipimo vya dactari ndivyo vitathibitisha dhahiri kuwa mtu huyo kalawitiwa au hapana.

Matokeo ya kufumbia macho ulawiti

Kosa la kulawiti lisipochukuliwa hatua au likafumbiwa macho na kuwalinda wale wanaofanya kitendo hiko cha kulawiti watu wengine ni kuendelea kuchochea mmomonyoko wa maadili na kutotii sheria za nchi.

Ktendo cha ulawiti hakina matokeo chanya, isipokuwa kina matokeo hasi wakati wote, kwa sababu kitendo cha kulawiti kina madhara kiafya, kijamii na pia kiuchumi.

Wataalam wa afya wanasema miongoni mwa athari au madhara yake ni kama, kuzalisha mashoga wengi ambao hawakubaliki katika jamii. Kupata maambukizi ya magonjwa kwa urahisi hasa kupitia michubuko.

Athari nyingine ni utanukaji wa njia ya haja kubwa, kushindwa kuzui haja kubwa kutokana na kulegea kwa baadhi ya misuli inayohusika kuzuia na kubana utoaji wa haja kubwa. 

Kuathirika kisaikolojia na kuendelea kutamani kufanya hivyo kila wakati hivyo kuzidi kupata madhara na kuwa katika hatari zaidi ya kushambuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kuambukizwa.

Pia kupata miwasho sehemu za haja kubwa kutokana na hali ya vidonda au michubuko.

No comments