HEADER AD

HEADER AD

SERIKALI YAPONGEZWA UKARABATI WA SOKO KUU ULIOGHARIMU MILIONI 114

>>Tsh Milioni 97 ni fedha za Mfuko wa Jimbo.

>>Milioni 17  fedha kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.


Na Samwel Mwanga, Maswa

UKARABATI unaoendelea  wa Soko Kuu lililoko mjini Maswa katika Halmashauri ya wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu uliogharimu hadi sasa Shilingi Milioni 114 umeleta faraja kwa Wafanyabiashara wa Soko hilo ambao kwa sasa watapata vizimba vya biashara zao ambavyo ni vya kudumu.

Hayo yameelezwa Agosti 9 Mwaka huu na Katibu wa soko hilo,Lucas Kahindi mbele ya Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Stanslaus Nyongo alipotembelea soko hilo na kuzungumza na Wafanyabiashara wa soko hilo.

   Katibu wa Soko la Mjini Maswa,Lucas Kahindi(aliyesimama)akisoma taarifa ya ukarabati wa Soko hilo kwa Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki,Stanslaus Nyongo(aliyekaa kushoto)

Ukarabati wa soko umetumia kiasi hicho Cha fedha zikiwemo Tsh.Milioni 97 kutoka mfuko wa maendeleo wa Jimbo la Maswa Mashariki na Tsh. Milioni 17 kutoka Halmashauri ya wilaya hiyo.

Amesema kuwa awamu ya kwanza ya ukarabati umekamilika kwa gharama ya Sh Milioni 59 kwa mchanganuo Sh Milioni 42 kutoka Mfuko wa Jimbo na Sh Milioni 17 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.

Kahindi amesema jengo la kuuuza nafaka limeanza kutumika na tayari Wafanyabiashara 33 wamepatiwa vizimba kwa ajili ya kufanya biashara na jengo hilo limepewa jina la BLOCK A NYONGO ambalo ni jina la Mbunge huyo kwa kutambua mchango wake mkubwa katika ukarabati wa Soko hilo.

Ameendelea kueleza  kuwa awamu ya pili ya ukarabati ni pamoja na ujenzi wa jengo lenye vizimba 30 ambapo umefikia asilimia 90  hadi sasa zimetumika T.sh Milioni 55 za Mfuko wa Jimbo hilo na litakapikamilika litakuwa mkombozi wa Wafanyabiashara hao.

Jengo lililokarabatiwa katika Soko Kuu la mjini Maswa


"Tuliteseka sana nyakati za masika kutokana na bidhaa zetu kuliweshwa na mvua kutokana na mabanda yetu ya Zamani kuwa yanavuja Maji wakati mvua ikinyesha kwa sasa Mbunge tutafanya biashara zetu katika Mazingira mazuri  na tunaomba ukarabati huu uendelee"

"Pamoja na ukarabati huu mkubwa ulioufanya mbunge wetu bado tuna changamoto ndiyo ambazo ni pamoja na soko kutokuwa na choo sambamba kutokuwepo na mifereji ya kutolea Maji ndani ya Soko hasa nyakati za mvua ambapo kunakuwa na madimbwi ya Maji,"amesema.

Mbunge wa Jimbi hilo Stanslaus Nyongo akizungumza na Wafanyabiashara hao amesema kuwa anaupongeza uongozi wa soko hilo kwa kuweza kusimamia vizuri fedha zote zilizotolewa kwa ajili ya ukarabati wa soko hilo na thamani ya fedha inaonekana.

    Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki,Stanslaus Nyongo akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko la Mjini Maswa mkoani Simiyu.

Amesema kuwa soko hilo kwa siku za nyuma  lilikuwa katika hali mbaya na ndiyo maana alitoa ahadi ya kulifanyia ukarabati lakini kutokana na kazi nzuri iliyofanyika ya ukarabati imempatia ili kuhakikisha soko hilo linakuwa la kisasa kutokana na kuwa ni Kitovu cha watu katika wilaya hiyo kupata mahitaji yao katika wilaya hiyo.

"Tulitoka fedha za mfuko wa jimbo kwa ajili ya ukarabati wa soko hili na nilipata wakati mgumu kutoka kwa wajumbe wa kamati ya mfuko huo wakidai hiyo fedha igawanywe ikafanye na shughuli nyingine za maendeleo ndani ya Jimbo letu,"

"Kitendo cha kuleta fedha hapa ni dalili njema kwani hapa ni kitovu cha watu kuja katika soko hili na kupata huduma mbalimbali kwani linatoa huduma kwa jamii hivyo ni lazima tulipe kipaumbele kwa kuwahudumia wananchi katika mazingira mazuri ili kuwaepusha watu kupata magonjwa ya mlipuko,"amesema.

Amesema kuwa zile changamoto zimeelezwa atahakikisha anazipatia ufimbuzi hata kupitia fedha zitakazotokana na vyanzo vingine vya mapato ili kuhakikisha soko hilo linakuwa la kisasa hata vibanda vinavyolizunguka soko hilo.

Aidha ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuendelea kulipatia fedha za kutosha katika Jimbo hilo kwani Kuna miradi mbalimbali inatekelezwa katika sekta ya Elimu,Afya,Miundombinu ya barabara,Maji,Kilimo na Mifugo,Umeme na Maendeleo ya Jamii.

Naye diwani wa Kata ya Sola,Masanja Mpiga ambapo ndipo Soko hilo lilipo aliuonba uongozi wa Soko hilo kuhakikisha wanalitunza ikiwa ni sehemu ya kuenzi mchango wa Mbunge huyo katika kuleta Maendeleo katika Jimbo hilo kwani amefanya mambo makubwa katika kipindi chake Cha Uongozi tofauti na Watangulizo wake.

Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki,Stanslaus Nyongo(mwenye taji)akiwa na baadhi ya Viongozi wa Soko la Mjini Maswa alipotembelea kuona ukarabati unaoendelea katika Soko hilo.

Jengo lililokarabatiwa katika Soko Kuu la mjini Maswa



No comments