HEADER AD

HEADER AD

WAKULIMA 210 WA ALIZETI WAWEZESHWA MAJEMBE YA KUKOKOTWA KWA NG'OMBE

Na Samwel Mwanga, Maswa

JUMLA ya Wakulima 210 katika wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu wanaojishughulisha na kilimo cha zao la Alizeti wataondokana na kutumia jembe la mkono baada ya kupatiwa majembe ya kukokotwa na ng'ombe maarufu kwa jina la Plau.

Majembe hayo yametolewa na Kampuni ya Lilian Kinyemi(ABC) Co Ltd ya mjini Maswa  inayojishughulisha na uongezaji thamani ya zao la Alizeti katika wilaya hiyo kupitia Mradi wa FEGGE unaofadhiliwa na Taasisi ya MEDA TANZANIA.

Akizungumza na Wakulima hao kwa nyakati tofauti tofauti wakati akikabidhi majembe hayo  Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Lilian Kinyemi amesema kuwa kwa kushirikiana na MEDA TANZANIA  wametoa fursa kwa wakulima kuwapatia majembe hayo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 46 ambayo ni ruzuku zinazolingana(Matching Grants).


Amesema kuwa Kampuni yake pekee imetoa kiasi cha Sh 21,728,750/-kwa ajili ya kununua majembe hayo na kiasi kilichobaki kulingana na uhitaji wa mkulima kitalipwa na mkulima.

Ameendelea kueleza kuwa motisha hiyo ambayo imesambazwa kwa wakulima ambao asilimia 72 ni Wanawake  waliopatiwa mafunzo awali juu ya kilimo cha Alizeti kutoka katika Vijiji vya Jihu ,Njiapanda, Mwamitumai, Mwawayi na Dodoma.

      Mwakilishi wa Kampuni ya Lilian Kinyemi(ABC),John Kinyemi akisoma  taarifa ya Mradi unaotekelezwa na Kampuni hiyo ya kilimo Cha Alizeti katika wilaya ya Maswa

Vijiji vingine ni pamoja na Hinduki ,Isulilo, Ngongwa,Kidema,Ilamata Lalago na Ng'hami.

"Sisi Kampuni ya Lilian KinyemiABC)tumetoka kiasi cha Shilingi Milioni 21.7 na kiasi kilichobaki kitachangiwa na Wakulima wetu ukiangalia hii ni motisha maana mzigo mkubwa tumeubeba sisi na lengo tuhakikishe mkulima wetu anaondokana na kilimo cha jembe la mkono,"amesema

Amesema kuwa iwapo mkulima atatumia zana za kisasa za kilimo na kuondokana na kilimo cha jembe la mkono na hatimaye wataongeza tija na kuwavutia vijana kwenye sekta hiyo.

       Baadhi ya Wakulima wa Alizeti katika Kijiji Cha Dodoma wilaya ya Maswa wakiwa wanasibiria mgao wao wa majembe ya kukokotwa na ng'ombe yaliyotolewa na Kampuni ya Lilian Kinyemi(ABC)ya mjini Maswa.

Amesema kuwa pia Kampuni hiyo imetoa mbegu bora za Alizeti kwa njia ya msaada kwa ekari moja kwa kila mkulima wa mwaka wa kwanza pamoja na mbolea kwa njia ya mkopo kwa Wakulima ambao walipokuwa tayari.

"Pia katika kupitia Mradi huo tumeweza  kutoa mashamba darasa tisa kwa wakulima hawa ili kuweka hamasa kwa Wakulima wengine kuweza kulima zao la Alizeti,"amesema.
        Mkulima wa zao la Alizeti,Hollo Ngalula Mkazi wa Kijiji Cha Dodoma wilaya ya Maswa akifurahia baada ya kukabidhiwa jembe la kulimia na Kampuni ya Lilian Kinyemi(ABC)ya mjini Maswa.

Aidha ametumia fursa hiyo kuwashukuru MEDA TANZANIA kwa kuweza kuwapatia nguvu za msaada wa fedha na kuunga mkono juhudi za serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu katika kupunguza umasikini na utegemezi katika jamii kwa kuwapa maarifa ya ujasiliamali,Usawa wa jinsia na Zana za Kilimo.

Baadhi ya Wakulima wa kijiji cha Dodoma ambao wamepatiwa majembe hayo wamehaidi kuongeza uzalishaji kwa ekari kutokana na kupata Zana za Kilimo za kisasa ambazo zitawarahisishia katika Kilimo kuliko Zamani walipokuwa wakitumia jembe la mkono.

       Afisa wa Taasisi ya MEDA TANZANIA, Denis Christian(mwenye miwani)akikabidhi jembe la kukokotwa na ng'ombe,Leticia Mtamula mkulima wa zao la Alizeti katika Kijiji cha Dodoma wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu.

"Nimetumia jembe la mkono kwa muda mrefu na mavuno niliyokuwa nayapata kwa ekari moja yalikuwa chini kutokana na kutumia jembe hilo ila kwa sasa nimepata jembe hili hii ni Zana ya kilimo ya kisasa ni matumaini yangu makubwa nitapata mavuno ya kutosha,"amesema Leticia Mtamula.

Naye Suzana Deus amesema kuwa alikuwa anatumika kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kukodisha jembe la kukokotwa na ng'ombe ili kuweza kulimiwa shamba lake lakini kwa Sasa fedha zake zitafanya shughuli nyingine ya palizi na siyo kulimia shamba tena kama ilivyokuwa awali.

        Mkulima,Suzana Shija wa Kijiji  cha Dodoma wilaya ya Maswa akiwa na jembe lake baada ya kukabidhiwa na Kampuni ya Lilian Kinyemi (ABC)ya mjini Maswa.

Pia wameomba wapatiwe mashine ndogo mdogo kwa ajili ya matumizi ya kukamua mafuta ya matumizi yao kwa kuwa vijiji vyenye mashine hizo ni vichache na vipo mbali na maeneo wanapolima hali ambayo inawafanya kupoteza muda mwingi kufuata ilipo mashine.

         Mwakilishi wa Kampuni ya MEDA Tanzania,Denis Christian akizungumza na Wakulima wa kijiji cha Dodoma(hawapo pichani) wilaya ya Maswa wanaojihusisha na kilimo Cha zao la Alizeti.

No comments