HEADER AD

HEADER AD

RC MTANDA AWAKUMBUSHA WALIMU KUJIANDAA KABLA YA KUSTAAFU UTUMISHI WA UMMA

 


Na Shomari Binda, Musoma

MKUU wa  mkoa  wa Mara  Said Muhamed Mtanda amewakumbusha walimu wanaotarajiwa kustafu kujiandaa  kabla ya kuachana na utumishi wa umma.

Akizungumza na walimu wanaotarajiwa kustaafu na wale waliostafu kwenye semina iliyoandaliwa na chama cha walimu (CWT) mkoa wa Mara.

Amesema kabla ya miaka 4 ya kustaafu ni muhimu mtumishi kupanga kupokea maisha mengine baada ya kustafu.

Mtanda amesema miaka hiyo ni mizuri kujipanga hata kama mtumishi hana kiwanja wala makazi kujipanga kupata makazi.

Amesema makazi yana umuhimu mkubwa kwa mstaafu na kuzingatia lakini akiwa na muda wa miezi 6 hawezi kuwa na muda wa kujiandaa na maisha hayo.

Mkuu huyo wa mkoa amesema yapo maswali ya kujiuliza kwa kipindi cha miaka 5 kabla ya kustaafu ikiwa ni pamoja na kupanga pakuweka makazi.

" Kuna mtu anafanya kazi zaidi ya miaka 30 mjini baada ya kustaafu anarudi kijijini hajanunua ardhi anakwenda kuanzisha ugomvi na familia kugombea ardhi.

" Lazima tukumbushane kujipanga mapema kabla ya kustaafu na hapa kwenye semina tujiulize unakwenda kuweka makazi wapi baada ya kustafu",amesema Mtanda.

Amesema wapo walimu ambao wanajiingiza kwenye mikopo humiza ambayo baadae inakuwa na athari kubwa baada ya kustaafu utumishi na kuwataka kubuni ujuzi wa namna pia ya kufanya.

Mtanda amesema kama kuna mwalimu anayesumbuliwa na mikopo umiza afike ofisini kwake kuweza kutatua changamoto zake ili kumuepusha mwalimu na mawazo ili aweze kufundisha.

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu ( CWT) mkoa wa Mara,Abdalla Malima amesema kila mwalimu ni mstafu mtarajiwa hivyo ni muhimu kupata semina ya maisha baada ya kustaafu.

       Mwenyekiti wa Chama cha Walimu ( CWT) mkoa wa Mara,Abdalla Malima

Amesema wameona umuhimu wa kufanyika kwa semina kwa walimu wanaotarajiwa kustafu na wale waliostafu ili kuweza kujiandaa.

Katibu wa CWT mkoa wa Mara Susan Shesha amesema mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda amekuwa msaada mkubwa kwa walimu na kuwasaidia katika masuala mbalimbali.

         Katibu wa CWT mkoa wa Mara Susan Shesha

Amewataka walimu kuitumia fursa ya mkuu wa mkoa kuweka milango wazi ya kuwasikiliza walimu kumfikia na kuweza kupata ushauri.

Baadhi ya walimu wanaotarajiwa kustafu na waliostafu wamesema wamepokea ushauri wa mkuu wa mkoa na kuahidi kuyafanyia kazi ili kutojiingiza kwenye matatizo.

Katika semina hiyo mada mbalimbali ziliwasilishwa kuhusu maandalizi ya kustafu utumishi wa umma kutoka PSSSF,Mwalimu Commercial Benk,Mwalimu mjasiliamali na Benk ya CRDB.

No comments