MWL. GEORGE NYAKITA : HIZI SABABU ZINACHANGIA UFAULU MBAYA SOMO LA HISABATI
>>Mwl George Nyakita kutoka Tarime amefanya utafiti na kubaini sababu za ufaulu mbaya somo la hisabati katika shule za msingi
>>Abaini madhara ya ufaulu mbaya somo la hisabati
>>Asema mapendekezo yake yakazingatiwa yatasaidia kupunguza tatizo la wanafunzi wa shule za msingi kufanya vibaya katika somo la Hisabati
Na Dinna Maningo, Tarime
UFAULU mbaya katika somo la Hisabati umekuwa ni changamoto kubwa inayorudisha nyuma sekta ya elimu na hivyo kusababisha Taifa kukosa wataalamu katika sekta mbalimbali kutokana na wanafunzi wengi kufeli mtihani wa somo la Hisabati wanapohitimu elimu ya shule ya msingi.
Kufeli somo la Hisabati kumesababisha pia kuwepo kwa waalimu wachache wanaofundisha somo hilo katika shule za msingi na kusababisha kuwepo na idadi ndogo ya walimu wa somo la hisabati.
Uchache wa walimu wa hisabati unasababisha mwalimu mmoja wa hisabati kufundisha madarasa zaidi ya matatu huku akifundisha masomo mengine hivyo wakati mwingine akijikuta akishindwa kumaliza mada katika madarasa anayofundisha.
Pia, somo la hisabati limekuwa likiwashinda wanafunzi walio wengi na kuliona ni somo gumu na hivyo wengi kukimbilia masomo ya sanaa huku somo la hisabati likikosa wapambe nakujikuta likipendwa na wanafunzi wachache.
Mwalimu George Nyakita
Sababu za ufaulu mbaya
Matokeo ya utafiti na uchambuzi wa taarifa uliofanywa na mwl.George umebaini kuwa njia za ufundishaji wa somo la hisabati katika shule za msingi hazina ufanisi kwani imebainika kuwa baadhi ya walimu wa Hisabati hutumia viboko sana kuwachapa wanafunzi.
Walimu wamekuwa wakidhani kuwa kumchapa mwanafunzi viboko ndiyo suruhisho kumbe wanawajengea watoto hofu na kufanya wanafunzi kuogopa kusoma somo hilo.
Mtafiti huyo anaeleza kuwa walimu wengi huongea na ubao hawatumii njia shirikishi yenye kumjengea mwanafunzi dhana ya kile ajifunzacho.
Utafiti umebaini kuwa Zana ya kufundishia na kujifunzi haitoshelezi mahitaji ya wanafunzi ambazo zingemjengea mwanafunzi kumbukumbu ya kudumu.
Anasema walimu wengi hawatumii zana za kufundishia hii hutokana na kutokuwa na uelewa wa matumizi ya zana au shule kutokuwa na uwezo wa kununua zana za kufundishia.
Pia, imebainika kuwa jamii imekuwa na dhana na imani potofu kuwa somo la hisabati ni gumu. Hii huwafanya wanafunzi kukata tama kusoma somo la Hisabati kwa kuwasikia ndugu na jamii inayowazunguka kuwa somo la hisabati lina wenyewe.
"Hali hii husababisha somo la hisabati kufundishwa na mwalimu asiye na maarifa na stadi za Hisabati kwani mwalimu yeyote hupewa somo hili ili kukamilisha ratiba hivyo hufundisha ili mradi tu" anasema Mwl. George Nyakita.
Utafiti umebaini kuwa watoto kukosa muda wa marejeo inachangia ufaulu mbaya somo la hisabati kwani somo la Hisabati huhitaji mazoezi ya mara kwa mara.
"Wanafunzi hukosa muda wa kutosha wa kufanya marejeo ya waliyojifunza kutokana na majukumu mbalimbali ya nyumbani kama vile shughuli za shamba kufanyishwa shughuli za biashara kama vile kutembeza barafu, karanga, maandazi, kufanya biashara minadani , kwenye masoko na magulio.
"Pia mambo ya utandawazi yanachangia wanafunzi kushindwa kufanya marejeo na hupoteza muda kucheza gemu, michezo ya mpira na kutizama TV" anasema.
Mwl. Nyakita anasema somo la hisabati halitiliwi mkazo katika madarasa ya chini, mara nyingi madarasa ya chini hufundishwa na walimu wazee, wajawazito, wanaonyonyesha na hawafatiliwi badala yake mkazo huwa madarasa ya mitihani tu.
Anasema baadhi ya walimu hawamudu kufundisha Hisabati kwasababu wengi wao walifeli somo la hisabati na wengine kupata alama ya D. Walimu wengi hufundisha somo hilo kwa kuhawirisha mafunzo ya huko nyuma tu, hawana stadi sahihi katika somo la hisabati.
"Kwa utafiti niliofanya nimebaini kila walimu 10 wa hisabati walimu watano walipata F ya Hisabati katika mtihani wa kidato cha nne, walimu 2 hawakusoma hisabati na walimu 3 ndio walifaulu tena kwa kiwango cha D na C, hali inayosababisha somo hili hufundishwa na walimu kwa uzoefu na sio weredi" anasema.
Kwa mujibu wa utafiti wa mwalimu huyo wa hesabu anasema baadhi ya walimu hawamalizi mada kutokana na sababu mbalimbali kwani baadhi ya mada hazifanikiwi kufundishwa, mwanafunzi humaliza darasa na kuingia darasa lingine akiwa hajafundishwa mada zingine.
"Hili ni tatizo kubwa baaadhi ya mada hazijirudii katika madarasa ya juu, hivyo mwalimu asipomaliza mada humfanya mwanafunzi kutosoma mada hiyo, akikutana na maswali hushindwa kujibu.
"Mwanafunzi hasipomaliza mada humpa ugumu mwallimu atakayempokea darasa la juu na kutomudu KKK kwa mwanafunzi inachangia kutomudu somo la Hisabati" anasema Mwl.George.
Madhara ya kufanya vibaya Hisabati
Mwal. Nyakita anasema kwamba sababu hizo zimepelekea Taifa kukosa wataalamu katika nyanja mbalimbali kama wahasibu, wahandisi na wengi wanaohusiana na hisabati, kwani ukishindwa kumudu hisabati pia hatoweza kumudu masomo ya sayansi.
Anataja madhara mengine ni shule kukosa walimu wa Hisabati, walimu mahiri wa somo hilo hali inayopelekea wanafunzi kutosoma somo la Hisabati na hivyo kukosa walimu wenye stadi za Hisabati na baadhi ya walimu wasio na stadi hufundisha somo hilo ilimradi tu ili kukamilisha ratiba.
Anasema baadhi ya watu hawamudu baadhi ya stadi za maisha " Zipo stadi za maisha zinazotegemea hesabu katika maisha ya kila siku hivyo kutokuwa na stadi sahihi za hesabu humfanya mtu kushindwa kumudu baadhi ya stadi za maisha kama vile biashara, kurudisha chenchi, kukadiria, kununua.
Mwl. George anasema madhara mengine ni kuwepo na mwendelezo wa kutofanya vizuri somo la hisabati kwani walimu mahiri hawatakuwepo.
Pia ukosefu wa wataalamu mbalimbali katika fani zilizohusisha somo la Hisabati umesababisha Taifa kuingia gharama kwa kuajiri wataalam toka nje ya nchi.
Nini kifanyike
Kwa mujibu wa utafiti alioufanya Mwl. George anasema ili kuondokana na ufaulu mbaya wa somo la Hisabati mapendekezo haya yakazingatiwa yatasaidia kupunguza tatizo la wanafunzi wa shule za msingi kufanya vibaya katika somo hilo ;
"Zana za kufundishia zitumike ipasavyo, walimu wajitahidi kumaliza mada kwa wakati, walimu wa Hisabati wawepo wa kutosha shuleni na somo la Hisabati lipewe umuhimu na kipaumbele kuanzia darasa la awali.
Anapendekeza kwamba walimu wasio mahiri katika somo la Hisabati wasipewe somo hilo kulifundisha, walimu wa Hisabati watambue uwezo wa wanafunzi wao kwani wapo wenye uwezo mkubwa na mdogo, pia wapo wanaojifunza haraka na taratibu.
Anasema Serikali itoe vifaa vya shule kwa wakati ikiwemo vitabu na vifaa vingine vinavyomwezesha mwalimu wa hisabati kueleweka kwa urahisi ikiwemo kiboksi cha zana za kufundishia somo la hisabati.
"Vyumba vya madarasa katika shule za msingi vijengwe ili kupunguza idadi kubwa ya wanafunzi katika chumba kimoja kwani hali hii humfanya mwalimu kushindwa kulimudu darasa vizuri.
"Wizara ya elimu izingatie ufaulu wa somo la hisabati katika mtihani wa kidato cha nne na sita wakati wa uteuzi wa wanafunzi kujiunga na mafunzo ya ualimu" anasema.
Anasema wazazi watenge muda maalumu kwa watoto wao kufanya marejeo ya yale waliojifunza shuleni pamoja na kutowapa majukumu mazito mara wawapo nyumbani na wawazuie kutazama TV vipindi visivyowajenga pamoja na michezo ya gemu isiyokuwa na tija.
Anasisitiza walimu watafiti njia sahihi na rahisi za kufundishia somo la Hisabati, Serikali iwajengee uwezo walimu wa Hisabati ili kuboresha ufundishaji wao.
Mtafiti anasema kuwe na mkazo katika madarasa ya chini kama darasa la pili katika ufundishaji na ujifunzaji wa somo la hisabati hasa katika orodha ya kuzidisha ili kuwajengea msingi mzuri katika somo hilo.
"Shule zianzishe baraza huru la wanafunzi kujadili mwenendo wa ujifunzaji wao , hii ni sambamba na kuweka kisanduku cha maoni na wanafunzi waelekezwe jinsi ya kukitumia katika swala la ufundishaji.
"Uwekwe utaratibu wa ukaguzi wa kila mwisho wa muhula kwa kila mwalimu kulingana na mada zake na endapo atagundulika kuwa yuko nyuma basi hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake"anasema Mtafiti.
Mtafiti huyo wa somo la hisabati anahimiza walimu wajengewe uwezo katika somo la Hisabati ili kuongezewa stadi na maarifa ya kutosha katika somo la hisabati.
"Mfano STEP, SAYANSI MAZINGIRA, hapa mwalimu huboresha uwezo wake katika ufundishaji kwa kutumia njia bora na matumizi sahihi ya zana" anasema.
Mtafiti anashauri kuwa halmashauri zinaweza kutumia Rasilimali zilizopo ili kusaidia walimu kujengeana uwezo, halmashauri wanaweza kujipanga na kutumia baadhi ya walimu wachache wenye uelewa zaidi ili kusaidia katika kujengeana uwezo, na walimu kukutana mara kwa mara ili kubadilishana uzoefu.
Mwl. George anasema utafiti huo ameufanya katika halmashauri ya mji Tarime uliohusisha wanafunzi wa shule za msingi, walimu, wazazi pamoja na viongozi waandamizi wa elimu.
Anasema utafiti ulilenga kujua sabababu za ufaulu mbaya somo la hisabati, madhara ya ufaulu mbaya na nini kifanyike kupunguza ufaulu mbaya.
Mtafiti alirejea pia taarifa ya uchambuzi wa maswali kutoka Baraza la Mitihani Tanzania ( 2018) .Taarifa ya uchambuzi wa maswali kutoka Baraza la Mitihani Tanzania (2021).

Utafiti wa mwaka 2023 uliofanywa na Mwalimu wa somo la Hisabati anayefundisha somo hilo darasa la 5-7, shule ya msingi Mturu, Kata ya Turwa, katika halmashauri ya mji Tarime mkoani Mara, Mwl. Gerge Mwangwa Nyakita mwenye uzoefu wa kazi ya ualimu kwa miaka 34, umebaini sababu mbalimbali zinazopelekea ufaulu mbaya wa somo la hisabati katika shule za msingi.

Pamoja na utafiti jitihada za mwalimu huyu zilianzia mbali. Mwaka 2009 alianzisha klubu ya Hisabati katika wilaya ya Tarime ambayo kazi yake ilikuwa ni kuinua na kuboresha kiwango cha ufundishaji na ujifunzaji.
Klabu hii ilifanya mashindano ya somo la hisabati na sayansi ngazi ya shule, kata na wilaya.
Kutokana na jitihada zake mwaka 2016 aliteuliwa kuwa mkufunzi wa somo la hisabati kwa shule za msingi kwa mwaka 2016/2017.
Mwalimu huyu aliendesha semina kwa walimu wa hisabati halmashauri ya mji wa Tarime. Na amewahi kuteuliwa na Afisa elimu na kupewa Kibari cha kuruhusu klabu aliyoianzisha kuendesha shughuli zake.
Post a Comment