HEADER AD

HEADER AD

MKUU WA MKOA WA SIMIYU ATENGULIWA

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Ismail Nawanda.

     Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Ismail Nawanda ambaye uteuzi wake umetenguliwa, Juni, 11, 2024

Rais Samia amemteua aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Momba, mkoa wa Songwe, Kenan Kihongosi kuchukua madaraka hayo ya ukuu wa mkoa wa Simuyu.

    Kenan Kihongosi ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu

Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharifa Nyanga inasema Rais amemteua pia Elias Daniel Mwandobo kuwa mkuu wa wilaya ya Momba.

Kabla ya uteuzi,  Mwandobo alikuwa afisa mwandamizi, ofisi ya Rais Ikulu. Amemteua Christopher Magala kuwa mkuu wa wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara, Magala anachukua nafasi ya Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Pia amemteua Gerge Hillary Herbert kuwa msajili wa mahakama ya rufani . Kabla ya uteuzi, Herbert alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani.

Sharifa amesema uapisho wa mkuu wa mkoa na msajili wa mahakama ya Rufani utafanyika tarehe itakayopangwa.

>>> Rejea

Taarifa ya kutenguliwa uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Ismail Nawanda.  imetolewa leo Juni, 11,2024 ikiwa ni siku moja imepita baada ya kuchapishwa habari Juni, 10, 2024 katika chombo hiki cha habari yenye kichwa cha habari kisemacho " MKUU WA MKOA ATUHUMIWA KUMWINGILIA KINYUME NA MAUMBILE MWANAFUNZI WA KIKE "

Na Mwandishi, Wetu Mwanza

MKUU wa mkoa katika moja ya mikoa Kanda ya Ziwa, anatuhumiwa kumwingilia kinyume na maumbile na kumlawiti mwanafunzi wa kike anayesoma katika chuo kikuu cha St. Augustine jijini Mwanza.

Inadaiwa kuwa, mwanaume huyo ambaye ni mkuu wa mkoa fulani nje ya mkoa wa Mwanza alitenda kosa hilo Juni, 02, 2024, majira ya saa 20:30 katika maegesho ya magari ya Bar, maarufu iitwayo THE CASK iliyopo jijini Mwanza, ambapo alimwingilia kinyume na maumbile mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 21, jina linahifadhiwa anayesoma shahada ya kwanza ya ugavi na manunuzi katika chuo hicho.

Juni, 03, 2024, majira ya saa 11.00 katika jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, alifika binti huyo akiomba kuonana na wahusika wanaoshughulika na haki za binadamu.

Waliomsikiliza katika jengo hilo walimshauri aende kituo cha Polisi Dawati la jinsia na watoto, ndipo alifika katika dawati hilo ngazi ya mkoa na kutoa malalamiko yake.

Taarifa zinasema kuwa mwanaume huyo alimfanyia tukio hilo la kikatili baada ya kumpigia simu kwa kutumia namba ambayo tunaihifadhi kwenda namba ya binti huyo nayo tunaifadhi na kumtaka afike katika Bar ya THE CASK kwa ajili ya mazungumzo lakini alipofika katika eneo hilo ndipo alielekezwa kuingia ndani ya gari aina ya Toyota Crown nyeupe ambayo hakuweza kuitambua namba za usajili.

Mwanafunzi huyo wa kike aliliambia Jeshi la Polisi kuwa alipoingia kwenye gari alimkuta mtuhumiwa akiwa ameketi kwenye kiti cha dereva na kuanza mazungumzo.

Mlalamikaji baada ya tukio hilo alielekea Malimbe katika hosteli ya wanafunzi wa chuo cha SAUT iitwayo South Village ambapo alivua nguo alizozivaa siku hiyo na kuziweka katika kapu la nguo chafu kisha kulala huku akisikia maumivu makali mwilini mwake na kuamua kumpa taarifa mama yake mzazi kwa kumpigia simu namba zinahifadhiwa.

Taarifa zinasema mama yake mzazi alimshauri akatoe taarifa hizo kwenye vyombo vya kisheria ili hatua ziweze kuchukuliwa, ndipo mlalamikaji alichukua uamuzi wa kutoa taarifa hizo katika dawati la jinsia na watoto mkoani humo ambapo alitoa maelezo yake kwa maandishi kisha kupelekwa hospitali ya SEKOUTOURE kwa uchunguzi wa kitaalam.

Taarifa zinasema kuwa awali mtuhumiwa huyo amewahi tena kumwingia kinyume na maumbile binti huyo Januari, 20, 2024 majira ya saa 20: 30 katika Bar ya THE CASK alipokutana nae kwa mara ya kwanza katika sherehe ya kuzaliwa ya mtu mmoja jina linahifadhiwa ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa ni mgeni mwalikwa kwenye sherehe hiyo.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa na mmlalamikaji walitambulishana na kupeana namba za simu kwa ajili ya kuwasiliana kwa simu. Katika mazungumzo yao wakiwa ndani ya gari la mtuhumiwa, mwanaume huyo alimsihi akubali kufanya nae mapenzi kinyume na maumbile lakini mlalamikaji alidai kuwa hajawahi kufanya kitendo cha aina hiyo.

Inaelezwa kuwa mtuhumiwa alizidi kumbembeleza na kumshawishi kuwa asiogope kwani kwa mara ya kwanza atasikia maumivu lakini baadae atazoea na kuahidi kumbadilishia hali ya maisha yake kiuchumi kwa kumpatia 500,000 kila mwezi na kumsaidia dada yake jina linahifadhiwa kupata ajira.

Taarifa zinasema wakati wanaendelea kuongea ndipo mwanaume huyo alimfunua sketi na nguo za ndani kisha kumlawiti huku akimtishia kuwa asiangaike kupiga kelele kwa sababu gari lake linafahamika na kuna walinzi wamelizunguka hivyo hawezi kupata msaada wowote.

Baada ya tukio hilo mwanaume huyo alifungua mlango wa gari na mlalamikaji aliondoka. Mmlalamikaji na mtuhumiwa waliendelea kuwasiliana kwa simu, Whatssap, jumbe fupi, video calls huku mtuhumiwa akimtumia fedha za kujikimu.

Taarifa zinasema kuwa, Februari 2024, mlalamikaji anakumbuka siku hiyo ilikuwa ziara ya Rais mkoani Mwanza, ambapo mtuhumiwa alifika Mwanza na kumpigia simu mlalamikaji na wakakutana hoteli ya RYNANS BAY.

Mtuhumiwa alimtaka mmlalamikaji kuwa anataka kuwa anafanya nae mapenzi kinyume cha maumbile. Mmlalamikaji alikataa kata kata na kwa hasira aliondoka chumbani bila maelewano.

Habari zinasema mtuhumiwa aliendelea kumbembeleza mmlalamikaji ili siku moja amkubalie ombi lake la mapenzi kinyume na maumbile. Ilipofika Juni, 02, 2024, ndipo mtuhumiwa alizidi kumbembeleza mmalamikaji wakutane ili waongee zaidi kuhusu jambo hilo.

Mlalamikaji aliamua kwenda Bar ya THE CASK akidhani mtuhumiwa alibadili nia yake, pengine anataka kuomba msamaha kwa kitendo cha kumuomba mapenzi kinyume na maumbile. Alipoingia kwenye gari ndipo alifanya tukio la ulawiti.

Taarifa zinasema Dawati la jinsia na watoto mkoani Mwanza lilianza uchunguzi wa tukio hilo na kumuhoji mmlalamikaji na kumpeleka hospitali ya SEKOUTOURE kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalam baada ya kupata PF3.

Imebainika kuwa katika taarifa ya kitaalam iliyotolewa na Daktari wa hospitali hiyo jina linahifadhiwa, ameeleza kuwa katika uchunguzi wake amebaini kuwa mmalamikaji ameingiliwa kinyume na maumbile kwa kuingiziwa kitu butu katika sehemu yake ya haja kubwa na hivyo kusababisha michubuano na maumivu.

Wataalam wa uchunguzi wa kisayansi Juni, 03, 2024 walifika katika chumba anachoishi mmlamikaji na kufanikiwa kupata nguo ambazo mmlalamikaji alizivaa siku ya tukio na vielelezo vingine ambavyo vinapelekwa kwa mkemia wa serikali Kanda ya Ziwa kwa uchunguzi zaidi.

Pia mmlalamikaji amechukuliwa sampuli ya mate yake kwa ajili ya uchunguzi wa DNA huku wakisubiri mtuhumiwa atakapokamatwa aweze pia kuchukuliwa vipimo hivyo kwa hatua zaidi za upelelezi.

" Ufuatiliaji umefanyika katika eneo la tukio kwa kuangalia picha za video za CCTV Camera iliyofungwa kwenye jengo la ROCK CITY ambapo imemuonesha mmlalamikaji akiingia kwenye gari iliyoegeshwa kwenye maegesho hayo na ilipofika saa 20: 48 anaonekana mmlalamikaji akiingia kwenye hilo gari baadae saa 21: 12 mmlalamikaji anaonekana akitoka kwenye hilo gari.

" Kisha majira ya 00 : 24 gari hilo linaonekana kwenye geti kwenye mwanga mkali linasomeka T 496 BND Toyota Crown nyeupe huku dereva aliyevalia kapero akitoka kwenye gari hilo kwa ajili ya kulipia ushuru wa maegesho " Taarifa zinasema.

Mlalamikaji ambaye pia ameshiriki katika kuangalia CCTV Camera hiyo pamoja na askari wa upelelezi alimtambua mtuhumiwa na gari na kuwaonesha askari wa upelelezi kuwa ndiye aliyemfanyia tukio la ulawiti na kuitambua hiyo gari ndogo kuwa ndiyo iliyotumika katika eneo la tukio.

" Simu ya mmalamikaji na CCTV Camera footage vinaandaliwa kwa ajili ya kupelekwa kwenye maabara ya uchunguzi wa kisayansi kwa uchunguzi zaidi. Kuhusu gari T 496 BND Toyota Crown imetumwa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mwanza ili kujua uhalali wa gari" inaelezwa. 

Mtuhumiwa wa tukio hilo bado hajakamatwa na upelelezi bado unaendelea. Mtuhumiwa amefunguliwa jalada la uchunguzi  MZR/CID/PE/74/2024.

No comments