KILUMBO AFUNGUKA KUHUSU PICHA ZA HARUSI YAKE ZILIZOSAMBAA MITANDAONI
Na Andrew Chale, Dar es Salaam
MWALIMU wa Muziki wa Dansi na mcheza Dansi mjini Arusha ambaye picha zake za harusi zimekuwa gumzo mitandaoni kuanzia Aprili 29, 2023, Kilumbo Steven amefunguka juu ya uwezo wake wa aina mbalimbali ya 'break dance' akiwa amepiga picha kichwa kikiwa chini na miguu juu akiwa na mke wake wa ndoa.
Akizungumza kwa njia ya simu na Mwandishi wa Habari hii, Break Dancer huyo kupitia mpango wake wa B Boy Kilumbo amesema kuwa amepata simu nyingi ikiwemo pia kuona wadau wakiposti picha zake hizo mitandaoni.
"Nimefanya densi ndani ya harusi yangu.
Lakini pia picha nyingi tulipiga sema hizo mbili za kusimama kwa kichwa chini ndo imesambaa zaidi mitandaoni, ila tumepiga picha nyingi.
"Watu wengi wameona picha zile lakini wamekuwa na maoni tofauti, mie ni kijana ambaye nina malengo makubwa kupitia kipaji changu, nataka kuendeleza uwezo wangu huu na hata kuwarithisha wengine."Amesema Kilumbo.
Amesema lengo lake kubwa ni kuanzisha shule maalum ya Break Dance kwa vijana wote wa kiume na kike ili kuongeza vijana wengine zaidi.
"Hapa Tanzania najulikana kwa vijana wengi na nimekuwa nikiwafunza kwenye Break Dance, lakini pia nimekuwa nikishiriki mashindano tofauti, ikiwemo shindano la Hip-hop Hasili na mwaka juzi nilikuwa mshindi wa kwanza.
Pia nimekuwa nikifanya mashindano kwa njia ya mtandao 'Online' Marekani na pia nchi zingine hivyo kwa sasa malengo ni kuona nafika mbali na pia kuacha alama.
Kilumbo amesema kuwa, yeye ni miongoni aliyeamua kufanya maisha yake Arusha ambapo pia mbali na kufanya Break Dance, lakini pia anajihusisha na masuala ya Utalii akifanya program ya 'Ngondi ya mtembezi' akitembeza Watalii maeneo mbalimbali.
Post a Comment