HEADER AD

HEADER AD

AWESO AAGIZA MRADI WA MAJI SIMIYU UFANYIKE USIKU NA MCHANA


>> Amteua Mhandisi Luesetula kuwa Meneja RUWASA Simiyu

 

Na Samwel Mwanga, Simiyu

 

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso ameagiza utekelezaji mradi wa Maji wa Mabadiliko ya Tabia Nchi katika mkoa wa Simiyu ufanyike usiku na mchana ili uweze kukamilika kwa wakati ambao chanzo chake ni Ziwa Victoria.

 

Waziri Aweso ametoa agizo hilo Septemba, 8 mwaka huu alipotembelea eneo ambalo mradi huo unatekelezwa kwa lengo la kuona hatua ya utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya Tsh. Bilioni 440 ambao utanufaisha wananchi wa wilaya zote zilizopo katika mkoa huo ambazo ni pamoja na Busega, Bariadi, Itilima, Meatu na Maswa.

 

           Waziri wa Maji,Jumaa Aweso(wa pili kutoka kulia)akitoa maelekezo juu ya utekelezaji wa Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria mkoani Simiyu


Baada ya kukagua hatua ya mradi huo alitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Mradi huo unatekelezwa na  Kampuni ya China Civil Engineering Constraction Cooperation kuwa kazi zinafanyika usiku na mchana ili ikamilike kwa muda uliopangwa.

 

“Mkandarasi unayetekeleza ujenzi wa mradi huu mkubwa wa maji wa Ziwa Victoria katika mkoa huu wa Simiyu hakikisha unafanya kazi usiku na mchana ili kazi hii ikamilike kwa muda uliopangwa kwani fedha yote kwa ajili ya mradi huu ipo,”amesema.

 

Amesema kuwa kulingana na uhitaji wa maji katika mkoa huo katika utekekezaji wa mradi huo ni vizuri kazi zikafanyika kwa masaa 48 kila siku ili kuhakikisha dhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani inakamilika.


      Eneo ambalo ujenzi umeanza wa Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria katika mkoa wa Simiyu

 

Pia ameelekeza kuwa wananchi na vijana wote wenye sifa ya kufanya kazi kutoka kwenye maeneo panapojengwa mradi huo mkubwa wa maji katika mkoa huo unafanyika utaratibu ili waweze kupata kazi wanazozimudu na siyo kuwatumia watu wengine kutoka nje ya mkoa huo.

 

“Huu mradi unatekelezwa katika mkoa wa Simiyu hivyo naelekeza kuwa wananchi na vijana wa mkoa huu wapatiwe kazi za kufanya wanazoziweza ili nao wapate ajira za muda na kuona manufaa ya kuwepo kwa ujenzi huu kwenye eneo lao tusiwapatie kazi tu watu wa kutoka nje ya mkoa huu,”amesema.

 

Mei 27 mwaka 2023 Serikali kupitia Wizara ya Maji kusaini mkataba wa Tsh Bilioni 169  na  Kampuni ya China Civil Engineering Constraction Cooperatin kwa awamu ya kwanza kwa ajili utekelezaji wa mradi huo.


           Waziri Jumaa Aweso (aliye kati) alipotembelea eneo la Nyangokolwa wilayani Bariadi unapotekelezwa mradi wa maji wa Ziwa Victoria

 

Waziri Aweso katika kutembelea mradi huo aliambatana na Naibu Waziri wa Maji Mhe Andrea Kundo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenan Kihongosi na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri.

 

Katika hatua nyingine Waziri Aweso amemteua Mhandisi Emmanuel Luesetula ambae alikuwa anakaimu nafasi ya Meneja wa Mkoa, Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijiji ( RUWASA) kuwa Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA)mkoa wa Simiyu.

 


 

No comments