CCM YATAKA UDHIBITI WANYAMA WANAOVAMIA MASHAMBA YA WAKULIMA
Na Samwel Mwanga, Meatu
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM)Taifa, Dkt. Emanuel Nchimbi ameiagiza serikali kuthibiti wanyama wakali Tembo na Viboko ambao wamekuwa wakivamia mashamba ya wakulima katika wilaya ya Meatu mkoani Simiyu.na kusababisha hasara kubwa kwa mazao na hata kuhatarisha maisha ya watu.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwandoya wilayani humo amesema kuwa wanyama hao husababisha hasara kubwa ya mazao na kuhatarisha maisha ya watu.
Katibu Mkuu CCM,Emanuel Nchimbi akiongea na wananchi wa kijiji cha Mwandoya, jimbo la Kisesa wilaya ya Meatu mkoani Simiyu.
Amesema kuwa matukio ya wanyama kuvamia mashamba ya wakulima na kuhatarisha maisha ya watu yamekuwa yakitokea katika maeneo ambayo yako pembezoni mwa hifadhi za wanyamapori.
Amesema kuwa ni lazima sasa serikali ikachukua hatua ya kuwadhibiti wanyama kwani hatua hiyo itasaidia kupunguza migogoro kati ya wanyama na binadamu ili kuhakikisha shughuli za kilimo zinaendelea katika maeneo hayo kwa mafanikio na bila usumbufu wowote.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Katibu Mkuu CCM,Emanuel Nchimbi katika kijiji cha Mwandoya wilaya ya Meatu mkoani Simiyu.
“Nimemwagiza Waziri wa Maliasili na Utalii, Pindi Chana kuhakikisha serikali inachukua hatua kuwadhibiti wanyama wakali ambao ni tembo na viboko wanaovamia mashamba ya wakulima na wakati mwingine kuhatarisha maisha ya wananchi na hiki kilio kimekuwa kwa wananchi wanaoishi pemboni na hifadhi zetu za wanyamapori."
“Ni lazima hatua zichukuliwe za kuwadhibiti wanyama ili kusaidia kupunguza migogoro inayojitokeza ya mara kwa mara baada ya wanyama hao kuvamia mashamba ya wakulima.
" CCM ndio tuna serikali tunahakikisha kuwa kilimo kinaendelea katika maeneo hayo kwa mafanikio makubwa na tena bila usumbufu na hatutaki wananchi kuwa masikini ”amesema.
Awali Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina amesema kuwa katika jimbo hilo lenye Kata 13 lakini Kata 10 ndizo uvamizi wa tembo na umekuwa ukifanyika kwenye mazao yakiwa shambani na hata majumbani na kusababisha hasara kwa wananchi kwa kupoteza mazao yao na wakati mwingine kusababisha vilema na vifo kwa wananchi.
Mbunge wa jimbo la Kisesa,Luhaga Mpina(mwenye kipaza sauti)akitoa changamoto zinazolikabili jimbo lake wakati wa ziara ya Katibu Mkuu CCM,Emanuel Nchimbi(hayupo pichani)katika kijiji cha Mwandoya wilayani Meatu.
“Leo nakataa rufaa kwako Katibu Mkuu CCM katika jimbo letu la Kisesa ambalo lina Kata 13 lakini Kata 10 ndizo zinauvamiazi wa tembo ambao wamekuwa wakivamia na kula mazao ya wakulima yakiwa mashambani na hata nyumbani ambapo wanavunja nyumba za watu na kusabisha vifo na wengine kujeruhiwa kwa kupatiwa vilema ".
“Wananchi wengi wameachwa katika hali mbaya ya umasikini licha ya serikali kujenga vituo vya kuwadhibiti tembo hao katika vijiji vya Ng’hanga,Malulu na Nyanza lakini bado uvamizi ni mkubwa.
" Kuna changamoto ya vifaa vya kuwafukuzia wanyama hao, havina uwezo mkubwa. Pia kutokuwepo kwa askari wa wanyamapori wa kutosha jambo ambalo limesababisha wananchi wangu wametiwa sana umasikini kwa zaidi ya miaka mitano. Tatizo hili halijapatiwa ufumbuzi hivyo nikuombe uiagize serikali ilimalize suala hili,”amesema mbunge.
Pia amesema kuwa serikali inapaswa kushirikiana na jamii zinazozunguka maeneo ya wanyama pori ili kutoa elimu juu ya mbinu za usalama na jinsi ya kuzuia uvamizi bila kuhatarisha maisha yao.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Katibu Mkuu CCM,Emanuel Nchimbi katika kijiji cha Mwandoya wilaya ya Meatu mkoani Simiyu.
Post a Comment