HEADER AD

HEADER AD

WAZIRI PINDI AZINDUA UTALII WA PUTO HIFADHI YA TAIFA RUAHA


Na Happiness Shayo, Iringa

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dkt. Pindi Chana amezindua rasmi utalii wa puto ikiwa ni maadhimisho ya miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa Ruaha. 

Uzinduzi huo umefanyika Oktoba 7,2024 katika eneo la Korongo View ndani ya Hifadhi ya Taifa Ruaha Mkoani Iringa.

Akizungumza katika mahojiano maalum ya Kipindi cha Jambo Tanzania ya Shirika la Utangazaji la TBC,  Pindi  amesema mafanikio hayo ni kutokana na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan  za kutangaza vivutio vya utalii.


"Tunamshukuru Rais Samia kwa kuionesha dunia vivutio vya utalii vya Tanzania ambapo mpaka sasa watalii wameongezeka na kufikia milioni 1.8 na mapato ya Taifa  tunachangia asilimia 17% na  fedha za kigeni takribani dola za kimarekani  Bilioni 3.6.

Kuhusu maboresho ya Miundombinu katika Hifadhi ya Taifa Ruaha Pindi amefafanua kuwa mpaka sasa kuna barabara ya Iringa- Msembe  yenye urefu wa kilomita 104 ambayo inaenda kujengwa.

Amesema katika Hifadhi ya Taifa Ruaha kutakuwa na uwanja wa ndege sambamba na kutumia uwanja wa ndege wa Nduli uliopo Mkoa wa Iringa ambao  unaendelea kukarabatiwa.


Ameongeza kuwa ndani ya miaka 3  kumekuwa na mabadiliko makubwa ya sekta ya utalii na serikali inazidi kuboresha maeneo mengi ya Utalii huku akihamasisha wawekezaji kujitokeza kuwekeza katika hifadhi hiyo.



No comments