MWENGE WA UHURU
NI kubwa yake thamani, mwenge wetu wa uhuru
Yapasa tuuthamini, umeangaza uhuru
Mwenge wetu wa amani, kila mtu yupo huru
Mwenge ni kielelezo cha Taifa letu huru
Mwenge ulitoa giza, na nuru ukaangaza
kutazama wapendeza, ndugu zangu nawajuza
Hakika unapendeza, si dhambi kuutangaza,
Mwenge ni kielelezo cha Taifa letu huru
Uliwashwa mlimani, nchi nzima ikapoa
Naeleza siutani, mwenge tulifurahia
Waliona majirani, Uganda na Kenya pia
Mwenge ni kielelezo cha Taifa letu huru
Udumu yote miaka, mwenge wetu wa thamani
Twajivunia hakika, mwenge wetu wa amani
Uliondoa mashaka, hata kule mipakani
Mwenge ni kielelezo cha Taifa letu huru
Tumaini ulitoa, kwa nchi ya Tanzania,
Dhuluma uliondoa, hata na unyonge pia
Mabaya ulikemea, na rushwa ukakemea
Mwenge ni kielelezo cha Taifa letu huru
Mwishoni naelekea, mengi nimeelezea
Shairi ninalitua, masikani narejea
Mwenge nimeelezea, ujumbe nimeutoa
Mwenge ni kielelezo cha Taifa letu huru
Mtunzi ni SirDody Dody - Kilimanjaro, 0762396923 au 0675654955
Post a Comment