HEADER AD

HEADER AD

VUNJENI MAKUNDI

MAKUNDI sasa vunjeni, na mariamu twendeni,

Na chuki ziondoeni, ninawajuza jamani,

Tumfanyie kampeni, hapo kondoa Mjini

Makundi sasa vunjeni na mariamu twendeni.

Hakika ni mgombea, ubunge kwetu jimboni,

Hana shaka mgombea, kura ni zake jimboni,

Mengi twayatarajia, tena yale ya thamani, 

Makundi sasa vunjeni na mariamu twendeni.

Mgombea wa thamani, tumempata kondoa,

Mwenye watu kuthamini, wazee vijana pia,

Ni kubwa yake thamani, huruma anayo pia,

Makundi sasa vunjeni na mariamu twendeni.

Jimboni utamlika, umeme na maji pia,

Mambo yatabadilika, maji atatuletea,

Kura za ndiyo hakika, mwana tutakupigia,

Makundi sasa vunjeni na mariamu twendeni.

Mizigo atatutua, kina mama wa kondoa,

Kwa maji kutuletea, kwa visima kupitia,

Kura utajipatia,  hofu sisi twakutoa,

Makundi sasa vunjeni na mariamu twendeni. 

Namaliza kuandika, shairi ninalitoa,

Mengi nimeyaandika, pembeni ninasogea,

Atashinda bila shaka, jimbo atalichukua,

 Makundi sasa vunjeni na mariamu twendeni. 

Sir dody Soyakijijini@ gmail.com

*0675654955*

No comments