HAMOUD JUMAA : NICHAGUENI NIENDELEZE MIRADI KIBAHA VIJIJINI
Na Gustaphu Haule, Pwani
MGOMBEA wa ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Jumaa ( Mzee wa Sambusa) amewaomba Wananchi wa Kata ya Mlandizi wamchague Oktoba 29 ili aende kushauriana na Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbalii ya maendeleo.
Jumaa amesema miongoni mwa miradi ambayo itakuwa ya kwanza kumshauri Rais Samia ni kuhusu ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Kibaha hadi Chalinze.
Mgombea ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa akiwa sokoni.Jumaa amesema mbali na hiyo lakini pia ameahidi kuisimamia barabara ya Makofia - Mzenga hadi Kisarawe ili iweze kujengwa kwa kiwango cha lami ambapo hadi sasa tayari barabara hiyo inajengwa kwa Kilomita 23 na mkandarasi yupo saiti( Site).
Jumaa ametoa kauli hiyo katika mkutano wake wa kampeni wa kuomba kura kwa Wananchi uliofanyika jana katika Kata ya Mlandizi mkutano ambao uliohudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka visiwani Zanzibar.
Amesema anatambua Rais ambaye ni mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt .Samia Suluhu Hassan amekaa madarakani miaka minne lakini amefanyakazi kubwa na imeonekana.
Amesema wanavyotaka aendelee kuwa madarakani sio tu kwasababu ya CCM wake lakini kwasababu ya kazi kubwa alizofanya katika kipindi hicho kifupi.
Mkutano wa CCM Kata ya MlandiziAmesema Dkt.Samia ameachiwa nchi katika kipindi kigumu na mtangulizi wake Hayyat John Magufuli lakini miradi yote ya kimkakati ambayo aliachiwa ameikamilisha vizuri.
Jumaa amesema Dkt .Samia aliachiwa mradi wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere lililopo Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani lakini ameweza kulikamilisha na sasa linafanyakazi kwa kuzalisha zaidi ya Megawati 2,115.
Jumaa amesema pia Dkt.Samia amemaliza mradi wa reli ya Mwendokasi kasi ( SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora Dodoma wenye Kilomita 722 ambapo kwasasa Watanzania unawasaidia katika kurahisisha safari zao.
Mgombea ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud JumaaAidha ,amesema Dkt.Samia ametimiza ndoto ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa kuhakikisha Mjini Dodoma unakamilika na amefanya hivyo kwakuwa wakati anaingia Dodoma ilikuwa imeachwa na vibanda lakini yeye ameikamilisha ujenzi wa ofisi zote na sasa Dodoma yamejaa Maghorofa kila kona.
Jumaa ameongeza kuwa chama kimeridhishwa na kazi ya Dkt .Samia ndio maana kimeona anafaa kuendelea kuongoza nchi kwa awamu nyingine kwahiyo ni vyema Wananchi sasa wakajitokeze Oktoba 29 kupigia kura za kihistoria kwa ajili ya kumchagua Dkt.Samia Suluhu Hassan.
"Niwaombe Wananchi wa Kata ya Mlandizi siku ya Oktoba 29 twendeni kwa pamoja tukamchague Dkt.Samia pamoja na mimi Hamoud Jumaa niwe mbunge wenu na bila kumsahau diwani Hamisi Sued ili kwa pamoja tukaunganishe nguvu ya kuwaletea maendeleo,"amesema Jumaa.
Mgombea udiwani wa Kata ya Mlandizi Hamisi Sued (CCM)amesema kuwa anatambua changamoto za Kata ya Mlandizi na kuwa akichaguliwa atakwenda kuzifanyiakazi kikamilifu.
Mgombea ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa ( aliyevaa kofia).
Post a Comment