Mfanyikazi wa Umoja wa Mataifa, raia wa Ufaransa ameuawa Goma

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amethibtihisha kuuawa kwa raia wa taifa hilo aliyekuwa mfanyikazi wa Umoja wa Mataifa katika shambulio jijini Goma, DR Congo.

Ufaransa imesema raia wake aliyekuwa akifanya kazi na shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu watoto UNICEF ameuawa kwenye shambulio la droni jijini Goma.
Ufaransa imesema raia wake aliyekuwa akifanya kazi na shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu watoto UNICEF ameuawa kwenye shambulio la droni jijini Goma. REUTERS - Stringer.

Kulingana na Rais Macron, Mfanyikazi wa shirika la kuwahudumia watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, ameuawa katika mashambulio ya ndege zisizo na rubani jijini Goma usiku wa kuamkia leo Jumatano.

Akituma salamu za pole kwa familia na mfanyikazi huyo wa UN, Rais Macron amezitaka pande hasimu mashariki ya Congo kuheshimu sheria ya kibinadamu kuhusu watoa huduma za kiraia na wafanyikazi wa mashirika ya misaada.

Ndege zisizo na rubani zilizotumika katika mashambulio hayo zilianguka katika Ziwa Kivu pamoja na makazi ya kibanfasi yalioko mita 50 kutoka nyumbani kwa Rais wa zamani wa DR Congo Joseph Kabila Kabange kulingana na ripoti ya shirika la habari la AP.

Makazi ya kibinafasi yaliolengwa jijini Goma katika shambulio la droni usiku wa kuamkia leo Jumatano.
Makazi ya kibinafasi yaliolengwa jijini Goma katika shambulio la droni usiku wa kuamkia leo Jumatano. REUTERS - Stringer

Msemaji wa waasi wa M23 ameituhumu serikali ya Kinshasa kwa kuhusika na shambulio hilo. Hadi tukichapisha taarifa hii, serikali haikiwa imezungumzia suala hili.

Tangu kuanzisha tena uasi mwaka wa 2021, M23 inayoungwa mkono na Rwanda imechukua Miji mikubwa miwili ya Bukavu na Goma nchini DRC.

matunda.

Kinshasa haijazungumzia shambulio hilo ambalo inatuhumiwa na M23 kutekeleza.
Kinshasa haijazungumzia shambulio hilo ambalo inatuhumiwa na M23 kutekeleza. REUTERS - Stringer

Mlipuko na mashambulio ya droni

Wanajeshi wa Congo wamekuwa wakiripotiwa mara kwa mara kutekeleza mashambulio ya droni za masafa marefu dhidi ya ngome za waasi wa M23 mashariki ya nchi.

Kulingana na vyanzo vya kiusalama, waasitt5 wa M23 nao pia wamekuwa wakiteleza mashambulio ya droni katika mstari wa mbele kwenye mapambano.

Kando na afisa huyo wa Umoja wa Mataifa, watu wengine kadhaa wameripotiwa kuuawa kwenye shambulio hilo.

Chanzo : RFI