HEADER AD

HEADER AD

NAIBU KAMSHINA WA TRA ZANZIBAR AWAHIMIZA WANANCHI PWANI KUDAI RISITI


Na Gustaphu, Haule Pwani

NAIBU Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar Salehe Pandu amewaomba Wananchi wa Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanadai risiti pale ambapo wananunua bidhaa ili kuisaidia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)kukusanya mapato.

Pandu amesema kitendo cha kudai risiti kinasaidia kupata taarifa ya kujua mfanyabiashara anafanya biashara yake kwa kiwango gani na anatakiwa kulipa kodi kwa kiwango gani kwani lengo sio kutoza tu kodi bali ni kutozakodi  inayostahili.

     Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar Salehe Pandu akifanya usafi katika kituo cha mabasi cha Chalinze Mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika maadhimisho ya miaka 30 ya kuanzishwa kwa TRA.

Pandu ametoa kauli hiyo Juni 25/2026 aliposhiriki zoezi la kufanya usafi katika kituo cha mabasi Chalinze pamoja na kutoa vifaa vya kuhifadhi takataka ( Dustbin), vyombo vya kupikia na vya kuhifadhia chakula kwa mama lishe wanaofanya shughuli zao katika kituo hicho.

"Hatutaki tumdhulumu mtu na hatutaki tumpendelee mtu, tunapofanya kitu  maana yake tutasababisha wananchi wote wawe sawa katika ulipaji wa kodi na kuchangia maendeleo ya nchi,"amesisitiza.

          Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Zanzibar Salehe Pandu (Kulia) akimkabidhi vifaa ya kuhifadhia chakula mama lishe wa Chalinze Mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya kuelekea kwenye maadhimisho ya miaka 30 ya kuanzishwa kwa TRA.

Amesema kitendo cha TRA kwenda kutoa vifaa hivyo na vyombo vya chakula sambamba na kushiriki kufanya usafi katika eneo hilo kinaonyesha namna ambavyo TRA inavyowathamini wananchi na kwa hali hiyo itasaidia kuwa na mwamko wa kulipa kodi kwa hiari.

"Kwa upande wetu pia tuna nafasi ya kutoa huduma za jamii kufanya usafi maeneo ya wafanyabiashara, kwahiyo leo hii tumekuwa hapa kushiriki usafi na kutoa vifaa vya usafi pamoja na vyombo kwa mama lishe tunataka nao wakue na kulipa kodi kwa kiwango cha juu", amesema.

        Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani Peter Jackson wa kwanza kulia akishika kontena za kuhifadhi chakula tayari kwa kuwakabidhi Mama lishe wa kituo cha mabasi Chalinze hafla iliyofanyika Juni 25/2026 .

Amewashukuru wafanyabiashara wa Mkoa wa  Pwani kwa kuwawezesha TRA kuvuka malengo kwenye makusanyo ya mapato hali ambayo imechangia kuwa na maendeleo kwenye sekta mbalimbali yaliyotokana na ulipaji wa kodi mzuri  .

Mwenyekiti wa Mamalishe katika kituo cha Mabasi Chalinze Zainab Bakari ameishukuru TRA Mkoa wa Pwani kwa kuwapatia vyombo vya kuhifadhia chakula, sufuria na vifaa vya usafi.

        Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani Peter Jackson aliyesimama akiwa katika zoezi la kufanya usafi katika kituo cha mabasi Chalinze Mkoani Juni 25/2026.

"Zamani tuliamini TRA kazi yao ni kufunga biashara lakini kwahiki mlichokifanya leo mmebadilisha dhana yetu na kutufanya tuone ni watu ambao tunaweza kuwashirikisha changamoto zetu hata tunapokwama ofisi yenu itatupatia ushauri wa kuendeleza biashara zetu," amesema

Naye Meneja wa Kituo cha mabasi Chalinze Henry Mwalugenge ameishukuru TRA Mkoa wa Pwani kwa kutoa vifaa hivyo huku akiahidi kuimarisha ushirikiano na Mamlaka hiyo katika eneo la kulipa kodi kwa hiari.

Mbali na Naibu kamishna huyo kukabidhi vifaa hivyo lakini pia alipata nafasi ya kutoa elimu vya kodi kwa wafanyabiashara waliopo ndani ya kituo hicho kwa kuwaomba kila mmoja alipekodi kwa wakati.

Hata hivyo,amrsema kila mfanyabiashara anapaswa kulipakodi kwa hiari hali ambayo itasaidia Serikali kutoa huduma kwa wananchi wake na kwamba kama kuna changamoto yoyote basi wawashirikishe watu wa TRA ili kuona namna ambayo wanaweza kutatua changamoto hizo kwa pamoja .

         Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani wakifanya usafi katika kituo cha Mabasi Chalinze ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika maadhimisho ya miaka 30 ya kuanzishwa kwa TRA.


No comments