HEADER AD

HEADER AD

MADAKTARI BINGWA KUTOKA CHINA WATUA MBEYA



 Na Mwandishi Wetu,Mbeya.

HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda Mbeya(MZRH), imepokea Madaktari Bingwa wanne kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ambao wanatarajiwa kutoa huduma mbalimbali za kibobezi, ikiwemo ya upasuaji kwa kushirikiana na Madaktari wa Hospitali hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt.Godlove Mbwanji amesema kuwa Madaktari hao watatoa huduma mbalimbali za kitabibu kwa wagonjwa mahututi, utoaji salama wa dawa za usingizi na ganzi, matibabu ya upasuaji wa watoto na upasuaji wa mifupa.

"Tunawakaribisha sana na tunaishukuru Serikali ya China kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na China katika sekta ya afya pamoja na Serikali yetu chini ya Rais wetu Samia Suluhu kupitia Wizara ya Afya kutuletea Madaktari Bingwa " alisema.
Aliongeza kuwa Madaktari hao watatoa huduma za kibingwa kwa kushirikiana na Madaktari wa MZRH kwa wakazi wa Nyanda za Juu Kusini na mikoa ya jirani" alisema Dkt.Godlove.

Kiongozi wa kundi hilo la Madaktari kutoka China, Dkt.Dubinbing ameushukuru uongozi wa hospitali ya MZRH kwa mapokezi mazuri na kuahidi kutoa ushirikiano mzuri kwa wataalam wa hospitali katika kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wa Tanzania. 



No comments