HEADER AD

HEADER AD

UBELGIJI: WATANZANIA CHANGAMKIENI FURSA YA BIASHARA NCHINI UBELGIJI



Na Jovina Massano, DIMA Online

WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia fursa za Biashara  ya mazao ya Samaki,Kilimo na Misitu nchini Ubelgiji pamoja na fursa za mikopo kwa ajili ya uwekezaji wa miradi mbalimbali  hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Jestas Abouk Nyamanga alipokuwa akiongea na Waandishi wa habari kupitia mtandao wa kijamii (ZOOM) Jijini Brussels. 

Balozi Nyamanga amesema kuwa fursa hizo zimetokana na ziara ya kikazi aliyoifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan alipotembelea nchini Ubelgiji  February mwaka huu ambapo alifanya mazungumzo na Waziri mkuu wa nchi hiyo Mh.Alexander De Croo na kukutana na wafanyabiashara wakubwa nchini humo.

"Hivi sasa kwa ujumla tunaingiza minofu ya Samaki aina ya Sangara kutoka kwa wafanyabiashara wa jijini Mwanza tani 50-60 kila wiki ambazo zinasambazwa hapa Ubelgiji na nchi nyingine ndani ya Umoja wa Ulaya kama tukijipanga tunaweza kuingiza zaidi ya tani 200 kila wiki tuendelee kuhamasisha Watanzania wenye uwezo wa kufanya Biashara ya mazao ya Samaki kuchangamkia fursa hii", alisema Nyamhanga.

Aliongezea kuwa, hivi sasa kuna soko jipya la mchele  tani 300  kila mwezi kutoka jijini Mbeya bidhaa nyingine ambazo zinazouzwa ni Parachichi,Dagaa,Kakao,Pilipili na Asali  kutoka kwa wafanyabiashara wa Tanzania.

"Wafanyabiashara wa matunda ya Parachichi aina ya hasi  rangi ya kijani yenye upele hii ina soko sana moja linauzwa kwa shillingi 10,000/= za kitanzania  wachangamkie soko na ili kuweza kufikisha sokoni kwa urahisi waonane na uongozi wa TAHA(Tanzania Hotcultural  Association) waliopo jijini Arusha kwa muongozo zaidi lakini hata kwenye bidhaa nyingine za mbogamboga.

"Kuna fursa pia za kuendeleza wajasiriamali wadogo zinazoilenga sekta binafsi zinazotolewa na Taasisi ya fedha ya BIO kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania  za upatikanaji wa mikopo nafuu chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya lakini pia utoaji wa mikopo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa nchi zinazoendelea ,ubalozi unatoa wito kwa wajasiriamali wa Tanzania kuchangamkia fursa hizi kwa kuwasilisha maombi yao.

Aliongeza kuwa fedha nyingi zimeelekezwa upande wa miradi ya uchumi wa Bluu na ili kufanikiwa kupata mikopo hiyo wahusika wanatakiwa kufika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupata utaratibu wa mikopo hiyo.


No comments