SHULE YA TARANGIRE KUTOA ELIMU YA THAMANI ENDELEVU
Na Mwandishi wetu, Babati
SHULE ya awali na msingi Tarangire ya mchepuo wa kiingereza iliyopo Wang’waray mjini Babati mkoani Manyara, imejipanga kuhakikisha inatoa elimu ya thamani endelevu kwa wanafunzi wake.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Babati, Mwalimu mkuu wa shule hiyo Juma Ama amesema lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu ya thamani endelevu ili wawe ni faida kwa Taifa hapo baadaye.
Mwalimu Juma amesema wanataka kuwapa elimu ya thamani endelevu wanafunzi hao ili waweze kujiamini na kujiandaa kupokea nchi na kuiongoza kwenye miaka ya baadaye.
Amesema wanafunzi wa shule hiyo wana uwezo mkubwa wa kujiamini na kujisimamia wao wenyewe hivyo wazazi, walezi na jamii kwa ujumla iwapeleke watoto wao wakapate elimu Tarangire.
“Shule ya Tarangire tumefungua soft opening Septemba 26 mwaka 2016 leo tumefunga miaka sita tunaaza mwaka wa saba,” amesema Juma.
Amesema wanafunzi wa shule ya Tarangire wanajiamini kutokana na elimu ya taaluma wanayoipata shuleni hapo kwani walishatoa madarasa matatu ya darasa la saba kwa ufaulu wa A.
“Tarangire tuna madarasa 10, mabweni mawili, magari na mabasi sita, wafanyakazi 32 na tuna wanafunzi 400 pamoja na ambao wanaohitimu darasa la saba mwaka huu,” amesema.
Ameongeza kuwa kupitia uwepo wa shule hiyo, majirani wa eneo hilo wameweza kupata maendeleo mbalimbali ikiwemo matengenezo ya barabara, nishati ya umeme, maji na mengineyo.
“Pamoja na hayo hivi sasa tunatarajia kuanzisha usharika wa Kanisa la KKKT ili tuweze kumtolea Mungu sadaka ya shukurani kwa mema yote aliyotujalia,” amesema mwalimu Juma.
Post a Comment