CHAMA KIPYA CHA WALIMU CHATAKIWA KUJITOFAUTISHA NA VYAMA VINGINE
Na Waitara Meng'anyi, Kigoma
CHAMA cha Kulinda na Kutetea Walimu Tanzania (CHAKUHAWATA) kimetakiwa kujitofautisha kiutendaji na vyama vingine vya wafanyakazi ili kufikia matarajio ya Walimu wengi nchini waliokata tamaa kwa kukosa msaada wa kutatua matatizo yao yanayowakabili kazini.
Agizo hilo limetolea na Mwenyekiti wa CHAKUHAWATA Taifa Mwalimu Kalmwambo Stephen Sabibi katika kikao kazi cha Makatibu na Kaimu Katibu wa Halmashauri,Mkoa, Manispaa na Majiji 32 Tanzania, kilichofanyika mkoani Kigoma Oktoba 17, 2022 katika ukumbi wa The wallet.
Amesema chama hicho cha walimu nchini ni kichanga lakini chenye nguvu kubwa kimetakiwa kujitofautisha na vyama vingine kiutendaji, kuwafanya Walimu wapate unafuu kimaisha hasa kipindi hiki cha mfumo wa bei za bidhaa na kupanda kwa gharama za maisha.
" Kujinyima Kwa viongozi na wanachama wa CHAKUHAWATA kila jambo kutakifanya chama hiki ambacho kimekuja kwa wakati wake kikaonesha tumaini kwa walimu nchini,utajiri wa mtu si fedha au mali bali watu alionao na sisi tuna watu," amesema Sabibi.
Amewataka wanachama kukosoa viongozi wa chama hicho kila wanapoona hawatendi ipasayo wakizingatia misingi, kanuni na katiba ya chama hicho huku
akiwataka kuendelea kukisimamia chama.
Aliyeketi ni Mwenyekiti CHAKUHAWATA Mwal.Kalimwambo Sabibi akiwa na viongozi wa chama hicho.
"Msitafute visingizio kwa kushindwa kwenu kutekeleza wajibu,acheni kuleana na kuteteana huku mambo yanaenda ndivyo sivyo, msiwaache wanachama wakahangaika kwa matatizo yao bali hakikisheni mnawasimamia wanapata haki zao," amesema Mwenyekiti wa chama hicho.
Katibu wa chama hicho mwalimu Twarib Nyamkunga amesema chama hicho ni mkombozi wa walimu nchini,"Nendeni mkasimamie vizuri chama katoka Halmashauri zenu kuelekeza walimu jinsi ya kujiunga na chama kwa hiari" amesema Nyamkunga.
Post a Comment