SERIKALI IMETOA BILIONI 2 KUJENGA VITUO VYA KUKUSANYA MAZIWA
Na Annastazia Paul,Simiyu
SERIKALI imetoa Shilingi Bilioni mbili zitakazotumika kujenga vituo 10 vya kukusanyia maziwa katika maeneo mbalimbali nchini ili kusaidia kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maziwa kitakachowezesha viwanda vinavyo sindika kuyapata kwa urahisi na kuongeza uzalishaji.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki amesema hayo Octoba,13,2022, alipokuwa katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu na kutembelea katika uwanja wa halmashauri ya mji wa Bariadi yanapofanyika maonesho katika uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya chakula duniani.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki
Waziri Mashimba ameeleza kuwa,kwa sasa uzalishaji wa maziwa nchini uko chini ikilinganishwa na lengo la uzalishaji wa maziwa ambapo nchi ya Tanzania inazalisha maziwa lita Bilioni 3.4, lengo likiwa ni kuzalisha lita Bilioni 12 kwa mwaka ili kutosheleza watanzania wote.
“Mwaka huu tunamshukuru sana Rais ametupatia pesa kiasi cha Tsh. Bilioni mbili ili tuweze kujenga vituo 10 vya kukusanyia maziwa kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini na mkoa wa Simiyu tutajenga kituo kimoja, ili wale wanaouza maziwa wawe na mahali watakapo yapeleka, tayakusanya maziwa haya ili yapelekwe kwenye viwanda yasindikwe yatumike kwa watanzania wote"Amesema Mashimba.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akinywa maziwa pamoja na wanafunzi
Msajili wa Bodi ya Maziwa Nchini
Dk. George Msalya amesema ni vema watu wakatumia maziwa yaliyosindikwa viwandani kwani yanajulikana ubora wake na ni salama kwa afya ya mtumiaji.
Wanafunzi wakipewa maziwa
"Yapo maziwa mengi sana hapa nchini katika mifumo isiyo rasmi, maziwa hayo hayatambuliki ubora yanauzwa kando ya barabara, mengine yanauzwa kando ya sheli za mafuta, si salama na yataleta madhara kwa walaji, tumesikia hata hivi karibuni kwamba maziwa yanaleta kansa, tuseme kwamba maziwa hayataleta kansa kama tu yataandaliwa kitaalam na kama yataandaliwa vizuri.
"Tutumie maziwa yaliyosindikwa kwani haya yanajulikana ubora kwasababu ndiyo maziwa salama kwa ajili ya afya zetu na nitoe wito tena kwa wazalishaji wa maziwa, tuendelee kuzalisha maziwa lakini tuyaelekeze haya maziwa katika viyuo rasmi vya kukusanya maziwa ili maziwa haya yafike viwandani, yasindikwe na tupate maziwa yanayokaa kwa muda mrefu na na maziwa ambayo ni bora na salama.” Amesema George.
Maonesho hayo leo yamekwenda sambamba na unyweshaji wa maziwa kwa wanafunzi toka baadhi ya shule za msingi mjini Bariadi ambapo mwalimu wa shule ya msingi Somanda B Saguda Ngulima amesema zoezi la unyweshaji maziwa ni muhimu kwani wanafunzi wanapokunywa mazi wanaongeza uwezo wa kulewa wanachofundishwa darasani.
“Kwa sasa unapofundisha wanafunzi wanakuwa hawaelewi kutokana na njaa lakini wakiwa wanapewa maziwa itasaidia kuwaongezea uelewa hivyo ni muhimu kwa wazazi kuhakikisha wanapata maziwa ili kuwajenga vizuri kiafya na kiakili pia.” Amesema mwalimu.
Emmanue Michael ni mwanafunzi wa shule ya msingi kidinda ameeleza faida za maziwa na kusema yanasaidia katika kuimarisha afya ya mtumiaji.
“Maziwa husaidia watoto sana katika kukua, himarisha mwili, kuwa na afya imara kwa sababu yanaimarisha mifupa na meno pia hutusaidia kuongeza kumbukumbu.” Amesema Michael.
Post a Comment