VYAMA VYA SIASA,ASASI VYAPATIWA ELIMU YA BIMA YA AFYA
Na Andrew Chale,Dar es Salaam.
VYAMA vya Siasa na Asasi za Kiraia Nchini vimepatiwa elimu ya uelewa juu ya Muswada wa Bima ya Afya kwa wote ambapo vimetakiwa kuwaelimisha wanachama wao juu ya dhana nzima ya Bima ya Afya.
Elimu hiyo imetolewa Oktoba 13, 2022 Jijini Dar es Salaam na Sekretarieti inayoshugulikia muswada wa bima ya afya kwa wote ikiongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Edward Mbanga
Mbanga amesema Serikali inataka wananchi wengi kuchangia bima ya afya kwa wote ili kuwasaidia wale wachache wenye matatizo ya kiafya kupata matibabu kupitia mfumo huo.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Edward Mbanga
Amesema kuanzishwa kwa mfumo huo utahakikisha wananchi watapata huduma za afya kwenye vituo vya afya kuanzia ngazi ya zahanati hadi Taifa.
"Wananchi watakaojiunga kwenye mfumo huo, watapata huduma bora kwani hivi sasa Serikali imeweza kuboresha miundombinu kwenye vituo vyake pamoja na kuwekeza kwenye vifaa tiba .
Katika Udhibiti wa huduma na fedha Mbanga amesema serikali inaweka mfumo thabiti wa kusimamia mifuko ya bima ya afya na kwamba ipo katika utaratibu wa uchambuzi wa kina ili kila taasisi itakayosimamia iweze kutekeleza kwa ukamilifu pasipo upungufu wowote.
Edward Mbanga akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa vyama.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo, wametoa maoni yao mbalimbali ambayo Kamati imesema imeyapokea.
Mwakilishi wa Chama Cha Mapinduzi-CCM kutoka Wilaya ya Ubungo (mwenye koti) akichangia mada juu ya semina ya uelewa wa bima ya afya kwa wote.
Baadhi ya Vyama vya Siasa vilivyoshiriki ni pamoja na Chama Cha CHAUMA, Chama Cha CCT, ACT Wazalendo, CUF, Chama Cha Mapinduzi-CCM na vinginevyo.
Mwakilishi wa Chama Cha CUF akichangia mada juu ya uelewa wa bima ya afya kwa wote.
Post a Comment