HEADER AD

HEADER AD

MZEE AKAMATWA KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 5

Na Annastazia Paul,Simiyu

JESHI la Polisi mkoa wa Simiyu linamshikilia mzee mwenye umri wa miaka 65 Mahona Mboje,mkazi wa kijiji cha Mpindo wilaya ya Maswa mkoani Simiyu kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka mitano ambaye ni mjukuu wake.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Simiyu ACP Blasius Chatanda amesema tukio hilo limetokea Oktoba 9, 2022 majira ya saa 10 jioni,alitenda tukio hilo wakati  bibi wa mtoto huyo akiwa  ameenda kuchunga mifugo huku  akieleza kiini cha tukio hilo kuwa ni tamaa za kimapenzi.

"Mtuhumiwa amekamatwa na yupo mahabusu kwa mahojiano na anatarajiwa kufikishwa mahakamani, nitoe wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujihusisha kimapenzi na watoto"amesema Chatanda.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua kali ikiwemo kifungo cha miaka 30 jela au kifungo cha maisha.

No comments