HEADER AD

HEADER AD

WAUGUZI MTWARA WALIOMTELEKEZA MJAMZITO WAKUTWA NA HATIA,WAFUTIWA LESENI


Na Andrew Chale,Kibaha 
 
BARAZA la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) limewakuta na hatia Wauguzi wanne wa Hospitali ya Mkomaindo mkoani Mtwara waliofikishwa kwenye kikao cha Baraza hilo, Kibaha mkoani Pwani ambapo limetoa adhabu kali ya kuwafutia leseni Wauguzi wawili huku wengine wakipewa onyo na kalipio kali.
 
Mwenyekiti wa Baraza hilo la Wauguzi na Wakunga Tanzania, Prof. Lilian Mselle amesoma hukumu mbele ya jopo la Wajumbe wa Baraza hilo sambamba na wauguzi hao pamoja na ndugu walioshitaki katika shauri la mwaka jana.

Wauguzi Tumaini Hussein Milanzi na Elizaberth Rashid Njenga wamekutwa na hatia kwa mujibu wa kifungu cha 25[3][K] cha sheria ya Uuguzi na Ukunga Tanzania, kwa kushindwa kutimiza wajibu wao wa kumuhudumia mgonjwa kwa kiwango kinachotakiwa sawasawa na alichojifunza.


Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania, Prof. Lilian Mselle akitoa maamuzi ya kesi 

Washtakiwa wote waliwasilisha utetezi wao pamoja na maelezo mengine ambapo mwenyekiti huyo alitoa onyo na kalipio kali kwa kila mmoja wao.
 
‘’Hukumu yako Tumaini na Elizabeth mmekutwa na adhabu ya kalipio kali, chini ya kifungu cha 28[3] [C], kwa maana hata ukija kufanya kosa dogo kiasi gani utachukuliwa maamuzi kwa kupata adhabu kubwa zaidi,’’ alisema Mwenyekiti wa Baraza hilo Prof. Lilian.
 
Prof. Lilian Masele, amesoma hukumu nyingine kwa Wauguzi Joyce John Mkane na Pascal Arudini Mnyalu, kwa pamoja walikutwa na hatia chini ya kifungu cha sheria cha 25[3][F] na kifungu cha 25[3][K] cha sheria ya Uuguzi na Ukunga Tanzania, kwa kosa la kumtelekeza mama Mjamzito aliyefika Hospitalini kwa lengo la kujifungua,
 
Pia kushindwa kudumisha viwango vya Kitaaluma, ambapo mgonjwa hakuonwa kabisa kitaaluma.
 
Katika utetezi wao Muuguzi Joyce aliomba kusamehewa adhabu kwa madai alishasimamishwa miezi kadhaa baada ya tukio hilo hivyo amejifunza kutokana na kosa, huku Muuguzi Pascal yeye aliomba asamehewa kwa kudai kuwa wakati wa tukio hilo alikuwa na changamoto ya kimahusiano kwenye familia yake na hivyo kupelekea kutofanya kazi kwa ufanisi.
 
Mwenyekiti Prof. Lilian Mselle ametoa hukumu juu ya shauri hilo, alisema 
Licha ya kuwasikiliza pamoja na utetezi wao, wanatoa hukumu hiyo ili kuwa fundisho kwa wengine.



 
‘’Wajumbe wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania wakiwa katika kikao hicho kabla ya maamuzi ya kesi ya Wauguzi  Hospitali ya Mkomaindo 

Nyote kwa pamoja, tumewapa adhabu ya kuwaondoa kwenye orodha ya Wauguzi na Wakunga kwenye Rejesta kwa mujibu wa kifu cha 28[3][A] cha Sheria ya Uuguzi na Ukunga Tanzania namba [1] ya mwaka 2010. 

"Kwa maana ya hukumu hii, hamtajishughulisha na shughuli za Uuguzi na Ukunga wakati wote mpaka pale wengine mtakapopata nafasi ya kukata rufaa kulingana na kifungu cha Uuguzi na Ukunga cha [31] ndani ya miezi mitatu,
 
" Rufaa hii inakatwa kwa Waziri mwenye dhamana, hivyo mtapewa kila mmoja nakala ya hukumu,’’ alieleza Prof. Lilian Mselle.
 
Hata hivyo kabla hajahitimisha tukio hilo, aliomba wote waliofikishwa hapo kumuomba msamaha mama mzazi ambaye mwanae aliyepelekwa kujifungua na kupelekea kifo cha mtoto.

‘’Kifo kinapangwa na Mungu na kinaweza kutokea ila kwa hali hii kingeweza kudhuhirika endapo wangefanya kazi zao kwa kuzingatia miiko.’’ Alihitimisha Prof. Lilian.
 
Ndugu waliopoteza mtoto wao, Wameishukuru Serikali pamoja na Baraza hilo kwa kuweza kutenda haki kwa wananchi wa kawaida wa Mtwara vijijini huku wakiomba wananchi wengine kuchukua hatua linapotokea tatizo lolote ambalo wataona halijaenda sawa katika masuala ya huduma za afya kutoka kwa Wauuguzi na Wakunga ama wengine.
 
Awali tukio hilo, lilitokea tarehe 1 na 2 Novemba 2021, saa tano usiku na siku iliyofuata ilidaiwa Wauguzi hao walishindwa kumuhudumia mgonjwa huyo ambaye alifika kituoni hapo kujifungua akitokea kituo cha Afya cha Kijijini.
 
Hukumu hiyo imesomwa mbele ya Wakili wa Serikali, Hangi Chan’ga , Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Prof. Lilian Mselle alisema Baraza limewatia hatiani walalamikiwa hao wanne huku mmoja akikutwa hana hatia 
 


 
Wakili wa Serikali akieleza vifungu vya Sheria katika hukumu hiyo

Msajili wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Nchini, Agness Mtawa amesema kuwa baada ya shauri hilo la Wauguzi kutoka Mtwara, pia wamepitia shauri la Wauguzi mkoa wa Arusha.
 

Msajili wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania, Bi. Agness Mtawa akizungumzia tukio hilo 

tuhuma mbili, moja mkoa wa Mtwara na moja mkoa wa Arusha, ambapo Baraza limeweza kutoa maamuzi hayo, ikiwemo kutoa kalipio kali na la kuwafutia leseni wauguzi,
Lakini pia kuna tuhuma tano ambazo bado tunaendelea kuzifanyia kazi. Nawaasa Wauguzi wenzangu kuzingatia sheria ili kuweza kutoa huduma bora.
 
"Lakini pia wananchi endapo wataona huduma hazijaenda sawa wasisite kutoa taarifa kwa baraza.’’ alisema Agness.
 

No comments