Home
/
MALIASILI/UTALII
/
WAZIRI PINDI CHANA : SERIKALI IMEDHAMILIA KUWAINUA WAFANYABIASHARA ZA UTALII
WAZIRI PINDI CHANA : SERIKALI IMEDHAMILIA KUWAINUA WAFANYABIASHARA ZA UTALII
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana amesema serikali imedhamiria kuwanyanyua wafanyabiashara za utali wa Tanzania kwa kuendelea kuandaa onesho la sita la utalii la Kimataifa.
Amesema onesho hilo linaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu za kuanzisha programu ya The Royal Tour Tanzania inayotangaza utalii wa Tanzania.
Dkt.Pindi ameyasema hayo wakati alipokutana na kamati ya Kitaifa ya maandalizi ya onesho la utalii la kimataifa linalojulika kama “Swahili International Tourism Expo (SITE)” kwa lengo la kupata taarifa ya maandilizi yanayofanywa na kamati hiyo.
Akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo, Dkt. Pindi amewasisitizia kujituma na kuhakikisha onesho hilo linafanyika kwa kiwango cha kimataifa ambalo linatarajia kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City uliopo jijini Dar es Salaam tarehe 21 hadi 23 Oktoba, 2022.
“Nategemea kuona taasisi zote za Wizara ya Maliasili zinahamasisha wadau wao kushiriki katika onesho hili na kutumia fursa hii kufanya biashara na wadau wa utalii kutoka nchi mbalimbali duniani waliothibitisha kushiriki katika onesho la mwaka huu”.
Ameongeza kuwa Kamati hiyo imepewa dhamana na kuaminiwa hivyo lazima kila mjumbe apambane kuhakikisha anatekeleza jukumu alilopangiwa na kwamba kamati hiyo imeshirikisha taasisi zote muhimu ambazo zina mchango mkubwa wa kufanikisha Site 2022.
Onesho la kwanza la Swahili International Tourism Expo lilifanyika mwaka 2014 katika Ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es salaam.
Post a Comment