OFISI YA URATIBU WA MIRADI YA UKIMWI YAFUNGWA
Na. WAF- Dar es Salaam
MENEJIMENTI ya Wizara ya Afya chini ya Katibu Mkuu Prof. Abel Makubi imechukua hatua za kuifunga Ofisi ya Uratibu wa Miradi wa Ukimwi, TB na Malaria (COAg) iliyopo chini ya Wizara ya Afya ambayo inasimamiwa na Dr Peter Mgosha kwa kukaidi agizo la Rais na Waziri Mkuu kuhamia makao makuu Dodoma.
Prof. Makubi ameifunga ofisi hiyo Desemba, 23, 2022, Jijini Dar es Salaam nakusema kuwa Dkt. Mgosha amekaidi zaidi ya mara tatu agizo la kuhamia Dodoma pamoja na kukumbushwa na Menejimenti ya Wizara.
Katibu Mkuu ameagiza watumishi wote wa ofisi hiyo wafike Dodoma Jumatatu bila kukosa.
Menejimenti imechukua hatua ya kufunga ofisi hiyo na hatua zingine za kinidhamu ziendelee chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu.
Post a Comment