HEADER AD

HEADER AD

KAMISHNA TFS PROF. SILAYO ATETA NA WADAU WA UHIFADHI

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

KAMISHNA Mhifadhi wa Misitu – TFS Prof. Dos Santos Silayo amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya Kiserikali PLAN VIVO Ms Fiona ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili umuhimu wa kushirikisha jamii na wenyeji katika uhifadhi wa bahari na pwani katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kupunguza utegemezi wa mazao ya mikoko.

Katika mazungumzo hayo Kamishna wa Uhifadhi ameihakikishia taasisi hiyo ya PLAN VIVO kuwa milango ipo wazi muda wote huku akiwaahidi kuwapa ushirikiano wakutosha katika kuhakikisha mikoko na pwani inahifadhiwa.

“Nikuhakikishie kwamba TFS itashirikina na asasi yako bega kwa bega kuimarisha usimamizi wa mikoko, na leo nakukabidhi kwa Mratibu wa Misitu ya Mikoko nchini Tanzania, Mhifadhi Mkuu Frank Sima ili muanze utekelezaji mara moja wa yale mliopanga kufanya  kwa ajili ya kuhifadhi mikoko lakini pwani pia,” anasema.

Akizungumza kuhusu ujio wake Ms Fiona aliyekuwa ameambatana na Diwani wa Kata ya Mchafukoge wilayani Ilala, Dar es Salaam Mariam Lulida amesema anakusudia kushirikiana na TFS katika usimamizi wa Hifadhi za Mikoko kupitia uanzishwaji wa shughuli mbadala za wanajamii kujiongezea kipato ili kupunguza utegemezi wa mazao ya mikoko.

Alizitaja shughuli hizo kuwa ni pamoja na unenepeshaji wa Samaki aina ya Kaa na Kilimo cha mwani.






No comments