HEADER AD

HEADER AD

CHADEMA YASISITIZA MALIPO KWA WAANDISHI WA HABARI


Na Jovina Massano, Musoma

WAMILIKI wa Vyombo vya Habari hapa nchini wametakiwa kuangalia maslahi na uwezesho kwa Waandishi wa Habari ili waweze kumudu shughuli zao za uandishi wa habari.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar,
Salum Mwalimu alipotembelea ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Mara (MRPC) mjini Musoma.

"Kumiliki chombo cha habari sio suala la kibiashara ni suala la umma, ili umma uweze kunufaika  na chombo chako lazima thamani ya waandishi ionekane wasiangalie kile wanachokipata kuwa faida yao pekee yao bila kujali maslahi ya waandishi", amesema Salum.

Kiongozi huyo amewakumbusha Waandishi wa Habari umuhimu wa kutumia vizuri kalamu zao kwa maslahi ya Taifa pamoja na  kuwa na mafunzo ya mara kwa mara ili kuongeza ufanisi katika kazi zao kuendana na mabadiliko ya teknologia.

     Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu

Ameongeza kuwa uandishi wa habari unatakiwa umakini wa hali ya juu na kujisimamia ili uwe na uhuru katika uhabarishaji kwa jamii.

Aidha Salum amezikumbusha Mamlaka kuwa habari ni muhimili wa nne nchini na hilo halina mjadala" Tuna Serikali, Mahakama, Bunge na inayofuata ni Habari hivyo  taaluma hiyo ni lazima iheshimiwe ipewe nafasi ya kutimiza majukumu yake kwa uhuru.


 "Changamoto zilizopo kwenye tasnia ya habari zisitumiwe kama fimbo ya kuwadhoofisha na kuwapunguzia nguvu na uwezo wa waandishi katika utekelezaji wa majukumu yao.

"Vyombo vya habari vipo  na ni vya muhimu vinatengeneza uhai wa Taifa kama hakuna vyombo vya habari hilo Taifa litakuwa mfu tu, ndio maana dunia ya leo unona teknologia zinalenga mambo mawili kurahisisha muda na upatikanaji na ufikiwaji wa habari",amesema Salum.

      Viongozi wa CHADEMA wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari ofisi ya MRPC mjini Musoma
            

No comments