RC MARA AAGIZA WENYEVITI, WAZAZI, NGARIBA WAKAMATWE
Na Jovina Massano,Tarime
MKUU wa mkoa wa Mara Meja Jenerali Suleiman Mzee, ameliagiza jeshi la Polisi mkoa wa Polisi Tarime Rorya kuwakamata viongozi wa vijiji, mitaa, Ngaliba na wazazi wa watoto 70 waliokeketwa baada ya kurejea majumbani kwao.
Watoto hao miongoni mwao walikimbia kukeketwa, walikuwa wakipatiwa elimu ya kupinga vitendo vya ukeketaji wakati wa rikizo mwezi Desemba,2022 katika Shirika lisilo la kiserikali la Association for Termination of Female Genital Mutilation (ATFGM) lililopo Kijiji cha Masanga Kata Gorong'a Wilayani Tarime.
RC Suleiman ameyasema hayo Januari, 10, 2023 wakati wa ziara yake ya kikazi katika vituo vinavyohifadhi watoto hao.
Rc MaraAmesema kuwa wazee wa mila waliongeza muda wa tohara na ukeketaji ambao kwa kawaida hustishwa mwishoni mwa mwezi Desemba.
Mkuu huyo wa mkoa amesema ni siku tatu tu tangu watoto hao watoke katika kituo hicho Cha ATFGM na kurejea makwao ili waende shule badala yake wamepelekewa kukeketwa.
"Nimeishakabidhi orodha ya majina ya watoto 70 wote waliokuwepo katika kituo hicho kuhakikisha wanawakamata na kufikishwa mahakamani." amesema RC Suleiman.
Amewataka viongozi kujitathmini katika utendaji wao huku akiwasisitiza kuhakikisha wanawachukulia hatua wahusika wa vitendo hivyo ili kumaliza ukatili.
Ameongeza kuwa katika msimu huo wa ukeketaji mkoa huo umewapokea watoto 750 waliokimbia kukeketwa.
Shirika la ATFGM Masanga linashughulika katika masuala ya kijamii ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu ya madhara ya ukeketaji na kupinga vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike.
Post a Comment