WANANCHI KUIBURUZA BARRICK NORTH MARA BARAZA LA ARDHI WILAYA
>>Yalalamikiwa kupora ardhi bila kulipa fidia
>>Yakacha kutembelea eneo la mgogoro
Mohere amesema Mdaiwa ambaye ni Mgodi wa Barrick uliowakilishwa na Afisa ardhi wa mgodi huo Ibrahim Nassoro alifika siku mbili tarehe 29,12,2022 na tarehe 05,02,2023 suluhu halikufanikiwa.
Mwenyekiti Mohere amesema mdai mwingine ni John Nyansika Matiko mwenye madai Na.08,2022 yaliyopokelewa kwenye Baraza na kuwakutanisha mdai na mdaiwa katika mgogoro wao.
Na Dinna Maningo, Tarime
BARAZA la Kata ya Nyamwaga Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara, limeshindwa kusuluhisha mgogoro wa ardhi wa walalamikaji wanne kati ya 25 wanaodai kuporwa mashamba yao na Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara yaliyopo Kitongoji cha Ntarachagini Kijiji cha Komarera kata ya Nyamwaga.
Akisoma madai ya walalamikaji na maoni ya Wajumbe wa Baraza Januari, 26, 2023, Mwenyekiti wa Baraza hilo la Kata Mohere Mwita Maricha, ameliambia Baraza kuwa suluhu halijapatikana baada ya mgodi kushindwa kutoa ushirikiano kwenye Baraza hilo hivyo Wajumbe wa Baraza kwa pamoja wamewatuma walalamikaji kwenda Baraza la ardhi la Wilaya ya Tarime kwa msaada zaidi wa kisheria.
Amesema walalamikaji hao walifungua shauri la madai Desemba,22, 2022 ambapo maombi ya madai Na.07/2022 kati ya Daniel Magige na Mgodi wa Barrick North Mara yalipokelewa kwenye Baraza la Kata la Nyamwaga tarehe 22,12,2022. Baraza limejaribu kuwakutanisha mdai na mdaiwa katika mgogoro wao.
Daniel Magige akiwa kwenye shamba lake la miti
Mdai na Mdaiwa mbele ya Baraza walikubaliana kutembelea eneo la mgogoro tarehe 13,01,2023, ilipofika tarehe hiyo mdaiwa hakufika wala kutoa taarifa, Baraza liliamua kwenda kutembelea eneo tarehe 17,01,2023 na kujiridhisha na majirani wanaozunguka eneo la mgogoro, hiyo ni kwasababu tarehe 5,01,2023 mdaiwa alisema eneo hilo halifahamu.
Amesema baada ya Baraza kufika Kwenye eneo la mgogoro na kujiridhisha na uhalisia wa eneo walikuta mashamba yamepandwa mazao ya kudumu, miembe komavu, mikaratusi na migomba ya ndizi
Pia Baraza lilikuta kipande cha shamba hilo kina namba za mgodi 1647 ambazo waliweka bila kulifanyia uthamini. Baraza lilikuta kipande cha eneo la mgogoro kimeanza kufunikwa na kifusi cha mawe na mgodi wa Barrick North Mara.
Mohere amesema Suluhu imeshindikana hivyo Baraza hilo limeamua kumtuma mdai Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya kwa maamuzi zaidi ya kisheria.
Mwenyekiti huyo wa Baraza amesema mdai Na.09,2022 Mwita Steven Waigama, maombi ya usuluhishi yalipokelewa kwenye Baraza hilo tarehe 22,12,2022, Baraza lilijaribu kuwakutanisha mdai na mdaiwa.
Mohere amesema Mdaiwa ambaye ni Mgodi wa Barrick uliowakilishwa na Afisa ardhi Ibrahim alifika siku moja tarehe 29,12,2022 na suluhu halikufanikiwa .
Amesema mdai na mdaiwa mbele ya Baraza walikubaliana kutembelea eneo la mgogoro tarehe 13,01,2023, ilipofika tarehe hiyo mdaiwa hakufika wala kutoa taarifa, Baraza liliamua kwenda kutembelea eneo tarehe 17, 01,2023 na kujiridhisha.
Imeelezwa kuwa Baraza lilipofika kwenye eneo la mgogoro lilikuta mdai ana mashamba matatu yenye vipimo tofauti na yote yamepandwa mazao ya kudumu, mikaratusi, miembe komavu, Migomba na matunda mengine mengi.
Mwenyekiti huyo amesema Baraza limekuta namba ndani ya shamba moja 1249 eneo la mgogoro. Kwakuwa mgodi haukutoa ushirikiano kuonesha mipaka ya eneo lao Baraza limeamua kwa pamoja kutuma mgogoro kwenye Baraza la ardhi na nyumba Wilaya ya Tarime.
Amesema mlalamikaji mwingine Amani Gugwa Chacha mwenye madai Na.10,2022 maombi ya usuluhishi yalipokelewa kwenye Baraza la Kata la Nyamwaga tarehe 22,12,2022.Baraza limejaribu kuwakutanisha mdai na mdaiwa katika mgogoro wao.
Amesema mdaiwa ambaye ni Mgodi wa Barrick uliowakilishwa na Afisa ardhi Ibrahim Nassoro alifika siku moja tarehe 29,12,2022 na suluhu haikufanikiwa .
Mwenyekiti amelieleza Baraza kuwa mdai na mdaiwa mbele ya Baraza walikubaliana kutembelea eneo la mgogoro tarehe 13, 01,2023, ilipofika tarehe hiyo mdaiwa hakufika wala kutoa taarifa. Baraza kwa pamoja lilipanga tarehe 17,01,2023 na tarehe hiyo ilipofika mdaiwa hakufika wala kutoa taarifa.
Ameeleza kuwa Baraza liliamua kwenda kutembelea eneo kulifahamu na kujiridhisha. Baraza lilipofika kwenye eneo la mgogoro lilikuta mdai ana mashamba na ndani ya mashamba kuna mazao ya kudumu kama vile Mikaratusi Komavu na Miembe komavu.
Baraza limekuta mdai huyo anatumia eneo lake kwa muda mrefu bila mgogoro na lalamiko lake limekuja baada ya mdaiwa kushindwa kutathmini eneo hilo,kwakuwa mgodi haukutoa ushirikiano kuonesha mipaka yao Baraza limemtuma mdai kwenda Baraza la ardhi Wilaya.
Ameliambia Baraza kuwa mdai na mdaiwa ambaye ni Mgodi wa Barrick uliowakilishwa na Afisa ardhi Ibrahim Nassoro alifika siku moja tarehe 29,12,2022 na suluhu haikufanikiwa .
Amesema mdai na mdaiwa mbele ya Baraza walikubaliana kutembelea eneo la mgogoro tarehe 13, 01,2023, ilipofika tarehe hiyo mdaiwa hakufika wala kutoa taarifa. Baraza kwa pamoja lilipanga tarehe 17, 01,2023 na tarehe hiyo ilipofika mdaiwa hakufika wala kutoa taarifa hivyo Baraza liliamua kwenda kutembelea eneo kulifahamu na kujiridhisha.
Mohere ameliambia Baraza kuwa Wajumbe wa Baraza walipofika Kwenye eneo la mdai huyo walikuta shamba hilo ni komavu na kuna miti aina ya Karatusi,miembe, miti ya limau na yote ilikuwa komavu.
Amesema ndani ya shamba hilo kulikuwa na namba 1284,1285, 1291,1293, 1297 na 1299 walishindwa kuzitambua kuwa ni za nani. Kwakuwa Mgodi haukutoa ushirikiano kuonesha mipaka yao Baraza limeshindwa kusuluisha mgogoro na kuamua kumtuma kwenda Baraza la ardhi na nyumba Wilaya kwa msaada zaidi wa kisheria.
Mwenyekiti huyo amewataja Wajumbe walioshiriki kusuluhisha mgogoro huo ni Mwenyekiti wa Baraza la Kata ya Nyamwaga Mohere Mwita Maricha, Gabrieli Mwita Rawe, Dorika Chacha Kirito.
Wengine ni Maswi Marwa Mohabe, Baru Mataiga Gikaro, Magoro Mseti Ntari, Gorge Nyanchama Bwana na Sauda Abdallah Keng'anya, barua ya madai imesainiwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo na Katibu wa Baraza Samwel Sabai pamoja na wajumbe.
Awali katika Baraza hilo ilidaiwa na walalamikaji hao kuwa Juni, 2022 maafisa wa mgodi waliingia kwenye mashamba yao bila ruhusa ya wamiliki wa mashamba na kuweka namba kwenye mawe na miti.
Walalamikaji wengine walidai kushuhudia namba kuwekwa kwenye mashamba yao lakini majina yao hayakuandikwa kokote wala kusaini na hawakupewa majibu ya siku, tarehe, mwezi wala mwaka wa kufanyiwa uthamini na malipo ya fidia.
Imedaiwa kuwa walalamikaji waliandika barua kwenda kwa Meneja Mahusiano mgodi wa Barrick North Mara kuomba kufanyiwa Tathmini lakini waliambiwa kuwa maeneo hayo yalishalipwa licha ya wao kukiri kutofanyiwa tathmini wala kulipwa fidia.
≥>Picha zote na Dinna Maningo
Post a Comment