MAWAZIRI, MAKATIBU WAKUU WAWASILI ITALY KUSHIRIKI MKUTANO WA IFAD
Na Mwandishi Wetu, Italy.
VIONGOZI Waandamizi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), wakiwemo Makatibu Wakuu wawili na Mawaziri wawili wamewasili mjini Roma nchini Italia kushiriki mkutano wa Baraza Kuu la Mfuko wa Maendeleo ya Chakula na Kilimo duniani (IFAD) unaotarajiwa kuanza Februari 13,2023.
Viongozi hao kutoka Wizara za Uvuvi na Mifugo, pamoja na ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi wanaongozwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Mashauri Ndaki ambaye ni Mkuu wa msafara huo unatarajiwa kuwakilisha vyema Serikali katika mambo mtambuka ya uvuvi.
Aidha, tayari ujumbe wa Serikali kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na na SMZ umepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Balozi Mahmmoud Thabiti Kombo pamoja na Maafisa wa Ubalozi huo wakiongozwa na Mwambata wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Misitu Jacquiline Mbuya Mhando.
Post a Comment