MILIONI 10 ZA UJENZI WA CHOO ZASOTA KWENYE AKAUNTI
Na Dinna Maningo, Tarime
WANAFUNZI na Walimu Shule ya Sekondari Inchage iliyopo Kijiji cha Soroneta Kata ya Nyarero, katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara wanatumia vyoo vibovu ambavyo si salama katika afya zao na ni hatarishi kutokana na ubovu wa vyoo hivyo.DIMA Online imebaini kuwepo kwa uzembe wa uongozi wa shule hiyo kuchelewa kujenga vyoo, kwani Halmashauri ya wilaya hiyo katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 ilitenga bajeti ya Tsh. Milioni 10.
Halmashauri katika mwaka huo wa fedha ilitoa kiasi hicho kwa ajili ya ujenzi wa maboma ya vyoo vya wanafunzi matundu 16 katika shule hiyo na fedha kupokelewa ambazo zimeendelea kusota kwenye akaunti ya shule pasipo vyoo kujengwa zaidi ya kuchimbwa mashimo mawili tangu mwaka jana.
Fedha zilizotolewa kujenga vyoo ni fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) zilizotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara.
Choo cha Wavulana
Post a Comment