HEADER AD

HEADER AD

CCM MIRWA YADAIWA KUTUMIA VIBAYA MADARAKA

Na Dinna Maningo, Butiama

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimeingia kwenye tuhuma ya matumizi mabaya ya madaraka kutokana na viongozi wa Chama Kata ya Mirwa kumkaimisha  mjumbe wa halmashauri ya Kijiji cha Magunga Daud Sarurya kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji.

Chama hicho kikiongozwa na Mwenyekiti CCM Kata Moris Onyango Odhiambo, Katibu Patrick Roche Pius kimempa majukumu mjumbe huyo kusimamia shughuli zote za serikali ya Kijiji ikiwemo miradi.

Mjumbe huyo amepewa madaraka hayo tangu chama hicho kilipomsimamisha uenyekiti Mwenyekiti wa Kijiji cha Magunga Magige Mahera Msyomi Novemba, 10, 11,2022.

Baadhi ya wajumbe wa Serikali ya Kijiji wakiwemo wenyeviti wa vitongoji wameshangazwa hatua ya CCM Mirwa kumsimamisha uongozi Mwenyekiti wa Kijiji huku halmashauri ya Kijiji ikiwa haijawahi kumjadili katika vikao juu ya tuhuma zilizodaiwa na CCM.

Pia hawajawahi kumshtaki kiongozi huyo kwenye chama chake cha CCM wala wananchi kumlalamikia Mwenyekiti huyo huku Wajumbe wengine  wakisimamishwa kazi bila kupewa barua.

Imeelezwa kuwa viongozi hao wanatumia vibaya madaraka kwa sababu ya maslahi binafsi ya kifedha katika miradi ya maendeleo kijijini humo pamoja na posho zinazolipwa kwenye vikao vya CCM ambazo ni pesa za miradi.

Wananchi wa Magunga wanashangazwa baada ya Diwani wao Willy Brown kumtambulisha mjumbe huyo kwenye msiba kuwa ndiye kaimu Mwenyekiti wa Kijiji huku wakihoji kuhusu taratibu za kichama na kiserikali za kusimamishwa uenyekiti, kukaimu na kutangazwa.

Wananchi  wanasema hawafahamu sababu ya Mwenyekiti kusimamishwa uongozi,na wanapofika ofisi ya kijiji wanahudumiwa na mtu mwingine ambaye hawajatambulishwa kwao kupitia mkutano mkuu.

Wananchi wanajiuliza kwamba mihtasari ya vikao na barua husainiwa na Mwenyekiti wa Kijiji je inayokwenda Halmashauri Wilayani husainiwa na kugongwa mhuri na nani?

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Butiama Patricia Kabaka amesema hana taarifa ya Mwenyekiti wa Kijiji kusimamishwa uongozi.

Je Viongozi wa CCM wanasemaje ? Na ni tuhuma zipi zinazomkabili Mwenyekiti aliyesimamishwa uongozi? Endelea kufuatilia DIMA Online.

No comments