HEADER AD

HEADER AD

RPC AELEZA UCHUNGUZI WA DAKTARI KIFO CHA MFANYAKAZI WA MGODI


>> Akanusha habari zilizoripotiwa mitandao ya kijamii zilizodai marehemu aliuawa kwa risasi

>>>Asema DIMA Online iliandika habari bila yeye kuthibitisha, DIMA Online yafunguka


Na DIMA Online, Tarime

KAMANDA wa Polisi mkoa wa Polisi Tarime Rorya ACP Geofrey Sarakikya amesema matokeo ya uchunguzi wa Daktari yamebaini kuwa kifo cha Mfanyakazi wa Mgodi wa Barrick North Mara, Emmanuel Chacha kimetokana na majeraha yaliyotokana na kujirusha kwenye shimo ndani ya mgodi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake Machi,20,2013, amesema kwamba kwa maelezo ya watu baki waliokuwepo kwenye eneo la tukio na matokeo ya uchunguzi wa Daktari katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza, uchunguzi umebaini majeraha yalitokana na kujirusha kwenye shimo hilo ambalo lina urefu wa takribani mita 20.

Kamanda huyo amesema kuwa ametoa taarifa hiyo kwakuwa Machi, 12, 03, 2023 alitoa taarifa ya kifo cha marehemu huyo aliyekufa kwa kujirusha chini ndani ya shimo (underground )mgodini majira ya saa 11 jioni.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Polisi Tarime Rorya ACP Geofrey Sarakikya

Amesema awali aliwaeleza waandishi wa habari kuwa baada ya uchunguzi wa Daktari atatoa taarifa.

Amekanusha taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii ukiwemo mtandao wa Twitter na Instagram wa DIMA Online kuripoti kuwa, kifo cha marehemu Emmanuel kilitokana na kupigwa risasi na kwamba taarifa hizo siyo za kweli na ukweli ni huo wa kiuchunguzi.

Baadhi ya Waandishi wa habari walitaka kuuliza maswali kuhusiana na taarifa hiyo lakini Kamanda Sarakikya alisema hataki maswali.

Machi, 12, 2023, saa 2: 55 asubuhi kupitia taarifa kutoka vyanzo vya habari DIMA Online iliripoti habari Twitter na Instagram, habari iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho 'MFANYAKAZI MGODI WA NORTH MARA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI '.

Habari hiyo ilisema; Mfanyakazi katika Mgodi wa North Mara, Emmanuel Mgesi Nyamaina(25) mkazi wa Kemakorere -Tarime, anadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na askari Polisi wanaolinda mgodi akiwa kazini eneo la piti ya Gokona usiku Machi, 11,2023.

Kabla ya kuripotiwa habari hiyo, majira ya saa moja asubuhi Machi, 12, 2023 Mwandishi wa DIMA Online alipokea taarifa kutoka kwa baadhi ya wananchi na ndugu wa marehemu wakieleza mfanyakazi wa mgodi kuuawa usiku kwa kupigwa risasi na polisi wanaolinda mgodi akiwa kwenye eneo lake la kazi maarufu piti ya Gokona.

Mwandishi huyo wa habari majira ya saa 2:30 asubuhi alimtafuta kwa simu Kamanda Sarakikya ili kutoa ufafanuzi lakini simu yake haikupokelewa.

Mwandishi alimtumia ujumbe wa maneno (SMS) muda wa saa 2: 32 asubuhi lakini ujumbe haukujibiwa.

Ujumbe huo ulisema " Habari Kamanda ?kuna mfanyakazi wa mgodi wa North Mara anadaiwa kupigwa risasi na Polisi akiwa kazini piti, naomba kufahamu hilo".

Hata hivyo Kamanda Sarakikya hakusema chochote, ilipofika mida ya saa 6: 13 mchana alimpigia simu Mwandishi huyo akilalamika kuandika habari kabla hajathibitisha, kwamba alipaswa kuacha kuandika habari ya tukio hilo hadi pale yeye atakapothibitisha.

Mwandishi alimweleza kuwa aliandika kile kilichoelezwa kupitia vyanzo vya habari kwakuwa alimpigia simu hakupokea na akamtumia sms hakujibu hivyo aliona aripoti kile kilichoelezwa na wananchi wakati huo akisubiri kupata taarifa ya RPC akihisi kwakuwa ni siku ya jumapili siku ya ibada huwenda yupo kanisani na atakapotoka atamjibu.

Mwandishi aliamini kuwa atakapotoka kanisani atakuta simu yake na ujumbe wa maneno na atampigia ili kumpa ufafanuzi kisha Mwandishi aripoti habari kwa mujibu wa Kamanda lakini hakutoa ufafanuzi wowote.

Kamanda Sarakikya hakuzungumza chochote kuhusiana na tukio hilo zaidi ya kumlaumu mwandishi kwamba ameandika habari ya uongo ambayo hajaithibitisha na kusema hawezi zungumza kwakuwa tayali mwandishi huyo ameshairipoti kisha alikata simu.

Baada ya Kamanda huyo kulaumu na kukata simu mwandishi huyo wa habari alimtumia tena ujumbe wa maneno (SMS)akimsisitiza azungumzie tukio hilo ujumbe huo ulisema;

"Mimi nimeandika kwa mujibu wa vyanzo vya habari kama ni uongo bado una nafasi ya kuongelea lakini umepiga umekata simu bila kuzungumzia na sms nilikutumia tangu saa mbili asubuhi, simu nikapiga hukupokea nikajua labda upo kanisani , nikajua kwakuwa utakuta simu yangu utapiga, mimi mtakuwa mnanilaumu bure.

"Bado unanafasi ya kuzungumza na nikaandika, maana nilichoandika ni kwa mjibu wa wananchi bado upande wako kama Kamanda una nafasi ya kuzungumza maana bado chanzo cha tukio hakijasemwa lakini nashangaa badala ubalance unapiga simu kulaumu kisha unakata bila kuzungumza" ujumbe wa Mwandishi kwa RPC.

Kamanda huyo hakumweleza chochote Mwandishi huyo hadi siku ya leo Machi, 20, 2023 alipomshirikisha kutoa ufafanuzi wa tukio la kifo cha marehemu.

No comments