MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI KUTEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA DAR
Na Andrew Chale, Dares salaam
MAKAMU wa Rais wa Marekani Kamala Harris anatarajiwa kutembelea Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam na kukutana na vijana wajasiriamali anayetarajia kufika tarehe 29 hadi 31 Machi 2023.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari nchini, kutoka Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imebainisha kuwa ujio wa Makamu huyo wa Rais wa Marekani ni kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"Kwenye ziara hii ya kwanza nchini Tanzania na barani Afrika, Kamala Haris anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika ujumbe wake Haris, watatembelea Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam na kukutana na vijana wajasiriamali wa Tanzania." Ilieleza taarifa hiyo.
Aidha, taarifa hiyo iliongeza kuwa, Pamoja na mambo mengine, ziara hiyo ya Haris inalenga kuongeza nguvu katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano nchi hizo mbili.
"Ziara hii inalenga katika kuunganisha nguvu za ushirikiano wa kimaendeleo kati ya nchi hizi mbili katika sekta za afya, kilimo, utalii, uchukuzi, uchumi wa buluu, mawasiliano, uchumi wa kidijitali.
Pia Uungaji mkono hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na uhimilivu wake na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kupitia ubunifu, ujasiriamali na uwezeshaji wanawake kiuchumi." Ilieleza taarifa hiyo.
Post a Comment