MWANAKIJIJI ASALIMISHA SILAHA BAADA YA KUPATA ELIMU YA UHIFADHI
Na Victor Meena, Iringa
MKAZI wa Kijiji cha Matalawe Kata ya Mlowa Jimbo la Isimani mkoani Iringa, amemkabidhi Silaha Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Godwel Ole Meing'ataki aliyokuwa akiitumia kufanya ujangili ndani ya hifadhi.
Mwanakijiji huyo amesema ameamua kusalimisha silaha hiyo aliyokuwa anaitumia kuwinda wanyama wa porini katika hifadhi hiyo baada ya kupata elimu ya ujirani mwema.
Amesema hayo wakati hifadhi hiyo ikitoa elimu ya uhifadhi na kupambana na vitendo vya ujangili kwa wananchi wa vijiji vinavyozunguka hifadhi.
Isimani mkoani Iringa, amemkabidhi Silaha Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Godwel Ole Meing'ataki aliyokuwa anaitumia kufanya ujangili
Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha, Godwel Ole Meing'ataki amesema zoezi la wananchi kusalimisha silaha zao kwa uwazi au kificho limeongezeka baada ya elimu inayoendelea kutolewa na mkuu wa hifadhi hiyo.
Godwel amesema ameamua kusimamia zoezi la kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi baada ya kuona hali ya ujangili inaongezeka.
Meing'ataki amesisitiza "Ni jukumu la kila mwananchi kujua umuhimu wa kulinda na kuhifadhi urithi tuliopewa na Mungu ili tuweze kuwarithisha watoto na wajukuu wetu kama ilivyo kauli mbiu ya uhifadhi isemayo "Tumerithishwa, tuwarithishe".
Ameongeza kuwa hadi sasa vijiji vilivyotembelewa na kupewa elimu ya uhifadhi ni pamoja na Kijiji Cha Kisilwa, Mahuninga, Makifu, Mapogoro, Idodi, Matalawe pamoja na kijiji Cha Tungamalenga ambacho ndicho kinachoongoza Kwa ujangili kwa mujibu wa tafiti.
Post a Comment