WANYAMA 700 HIFADHI YA MIKUMI HUPOTEZA UHAI WAVUKAPO BARABARA
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
HIFADHI ya Taifa ya Mikumi iliyopo Mkoani Morogoro imetoa raia kwa madereva kuzingatia sheria za barabarani ili kuzuia vifo vya Wanyamapori ndani ya hifadhi hiyo.
Hayo yameelezwa na Afisa Mwandamizi na Mkuu wa kitengo cha Utalii wa Hifadhi hiyo, Herman Mtei wakati wa ziara ya wadau kutoka Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) na baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari nchini.
Kwa mujibu wa Herman Mtei ametoa raia kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kunusuri uhai wa Wanyamapori ambao amesema ni tunu ya taifa.
"Ajali za barabarani si tu zina gharimu uhai wa wanadamu la hasha! hata uhai wa Wanyamapori nao uko mashakani kutokana na ajali za barabarani.
"Hifadhi ya Mikumi wanyama 700 kila mwaka wanapoteza uhai kwa kugongwa na magari ambayo yanapita katika hifadhi hii, hivyo tunaomba madereva kuzingatia sheria za barabarani ilikunusuru uhai wa wanyama." Amesema Mtei.
Amesema kiasi cha kilomita 50 za hifadhi hiyo zimepitiwa na barabara kuu ya Morogoro -Iringa ambayo wakati wote inatumika na magari makubwa na madogo.
Ameongeza kuwa,kupita kwa magari hayo mahali hapo, kumekuwa kukisababisha vifo kwa wanyama wanaovuka barabara kutafuta mahitaji mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maji na chakula, kutokana na kugongwa.
Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), sambamba na baadhi ya wahariri walifika katika hifadhi hiyo na kujionea hali halisi.
Post a Comment