HEADER AD

HEADER AD

KIVUKO CHASABABISHA KERO KWA WATUMIAJI WA BARABARA

Na DIMA Online, Tarime

BARABARA ya Komaswa-Nyamongo maarufu German Road wilayani Tarime mkoani Mara imekuwa kero kwa wananchi na watumiaji wa vyombo vya moto yakiwemo magari ya mizigo ya Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara kushindwa kuendelea na safari.

Ni baada ya kuharibika  kivuko kinachounganisha Kijiji cha Nyarwana na Nyakunguru Kata ya Kibasuka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na hivyo kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara.

Pia inalezwa kuwa Kivuko hicho kinahitaji matengenezo au kujengwa Kivuko kipya kutokana na kivuko hicho kujengwa kwa miaka kadhaa iliyopita.

Meneja Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) wilaya ya Tarime Mhandisi Charles Marwa amesema TARURA haihusiki na barabara hiyo na kwamba wahusika na wasimamizi wa barabara ya German ni Mgodi wa North Mara unaomilikiwa na Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya Barrick .

No comments