MWANDISHI BURUNDI ASEMA NI MUHIMU KUTANGAZA UTALII
Na Dinna Maningo, Mara
MWANDISHI wa Habari na Mtangazaji katika kituo cha Redio na Television (TV) cha Buntu nchini Burundi, Bankuwiha Elias Anthony amesema ni muhimu kutangaza Utalii kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kwakuwa vinasaidia kuchochea watu kutembelea vivutio vya kitalii.
Akizungumza na DIMA Online Bankuwiha ambaye pia anaripotia redio Kwizera iliyopo wilaya ya Ngara mkoani Kagera nchini Tanzania, amesema Utalii unasaidia nchi kupata fedha za kigeni ikiwemo Serikali na sekta binafsi.
"Binafsi naishukuru sana Kampuni ya Utalii ya Awesome Expedition kwa kuandaa kongamano la kuhamasisha Utalii mkoa wa Mara nchini Tanzania litakalofanyika Mei, 22-28,2023 na kuwashirikisha waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali.
"Nimefurahi sana kwa mwaliko huo niombe tu Mungu atujalie uzima na afya tele,mimi kama Mwandishi wa Burundi tutarusha matangazo ya moja kwa moja na nitaandaa vipindi mbalimbali ambavyo vitarushwa kwenye redio na TV Buntu.
Ameongeza" Vipindi hivyo vitawezesha wananchi wa Burundi kujifunza mengi kupitia kongamano hilo na nina imani Warundi wataitembelea Tanzania kujionea vivutio vya mkoa wa Mara" amesema Bankuwiha.
Bankuwiha amesema yeye si mgeni Tanzania kwakuwa alishawahi kuishi Musoma miaka kadhaa iliyopita na kwamba amefurahi kuwepo kongamano la kuhamasisha utalii katika mkoa huo wa Mara.
Mwandishi wa Habari na Mtangazaji katika kituo cha Redio na Television (TV) cha Buntu nchini Burundi, Bankuwiha Elias Anthony
"Naifahamu Musoma nimewahi kuishi, nitaisaidia Tanzania kutangaza vivutio vyake katika upande wa utalii, pia vyombo vya habari navyofanyia kazi naweza kusema ni nafasi chanya na ni fursa nzuri ya kupata habari nje na ndani tena zenye uhakika.
"Wanamara nikifanikiwa kuja naombeni ushirikiano wenu ili kufanikisha jambo hilo la kutangaza vivutio vya mkoa wa Mara.
"Abantu bo muntara ya Mara mugihugu cha Tanzania tuzoba turikumwe Musoma kuvuga nogutangaza ivya Mukerarugendo-(lugha ya Kirundi)"
Post a Comment