JAMII YATAKIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUPAMBANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO
Na Daniel Limbe,Chato
WIZARA ya afya kwa kushirikiana na shirika la Afya duniani (WHO) wameitaka jamii kushirikiana na serikari katika mapambano dhidi ya magonjwa ya milipuko ili kunusuru vifo vinavyoweza kutokea.
Aidha makundi ya waganga jadi na tiba mbadala,wazee maarufu,viongozi wa dini,wanahabari,wanafunzi na viongozi mbalimbali wa kijamii na serikali kwa ujumla, wanatajwa kuwa muhimu katika mapambano dhidi ya magonjwa ya milipuko nchini.
Wajumbe wa kamati ya RCCE Wilaya ya Chato,wakiendelea kupokea maelekezo kutoka kwa mwelimishajiKauli hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu kuripotiwa ugonjwa wa homa ya "Marburg" mkoani Kagera, ambapo watu kadhaa waliripotiwa kupoteza maisha huku wengine wakiwekwa karantini kwaajili ya uchunguzi zaidi.
Kutokana na hali hiyo, serikali kupitia wizara ya afya kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani (WHO) wamelazimika kuyafikia makundi hayo muhimu ili kuyajengea uwezo pamoja kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo, kipindupindu, Uviko 19 pamoja na homa ya Marburg.
Akizungumza na wajumbe wa kamati ya uelimishaji,uhamasishaji na ushirikishaji jamii (RCCE) wilaya ya Chato mkoani Geita, Ofisa progaramu wizara ya afya Idara ya kinga na elimu kwa Umma, Magdalena Dinawi,amesema jamii inapaswa kuwa bega kwa bega na serikali ili kuyafikia malengo yanayokusudiwa.
Ofisa programu kutoka Wizara ya afya,Idara ya kinga na elimu kwa Umma, Magdalena Dinawi,akizungumza na wajumbe wa RCCE hawapo kwenye picha."Wilaya ya Chato ni miongoni mwa wilaya zilizo karibu sana na nchi jirani za Uganda,Burundi na Rwanda na mwingiliano wa watu wetu ni mkubwa sana ndiyo maana Wizara ya afya tukaona ipo haja kwa mkoa wa Geita kuwajengea uwezo ili wasaidie kuifikia jamii iliyoko chini kuwaelimisha namna ya kuepukana na magonjwa ya milipuko".
Kadhalika amesema wilaya ya Chato inayo makundi mengi yenye mikusanyiko wakiwemo wachimbaji wadogo wa madini,wavuvi wa samaki,Magulio,wanafunzi,waumini wa madhehebu mbalimbali,waganga wa jadi pamoja na wasafiri na wasafirishaji abiria.
"Tunaamini tukielimisha wachache nao wataenda kuelimisha wengine wengi zaidi, lengo letu kubwa likiwa ni kuhakikisha wananchi wanaelimika kwa kuzingatia taratibu na kanuni zinazopaswa kufuatwa na kila mmoja wetu" amesema Dinawi.
Ofisa elimu afya kwa Umma na Afya ya akili kutoka shirika la afya Duniani (WHO) Jerry Mlembwa,amesema moja ya malengo muhimu ya shirika hilo ni kuhakikisha usalama wa jamii na kwamba bila ya jamii kuwa na afya bora itakuwa ni ndoto kufikia malengo mengine.
Ofisa Elimu afya kwa Umma,na Afya ya akili,kutoka WHO Jerry Mlembwa,akizungumza na vyombo vya habariKutokana na hali hiyo,ameisisitiza jamii kuungana kwa pamoja kukabiliana na magonjwa ya milipuko kabla na baada ya kutokea kwa kubadili mitindo ya maisha ikiwemo kusalimiana kwa kushikana mikono, kusogeleana karibu zaidi na kujiepusha na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima.
"Niwashauri ajenda ya magonjwa ya mlipuko inapaswa kupewa kipaumbele kwa kila vikao vyenu kwenye halmashauri ni muhimu pia kuwashirikisha wadau wenu wa maendeleo katika mapambano ya magonjwa ya mlipuko sisi kama WHO tupo tayari kuzisaidia nchi wananchama ikiwemo tanzania kwenye magonjwa hayo" amesema Mlembwa.
Kwa mujibu wa Mganga mkuu wa wilaya ya Chato,Dk. Eugen Rutaisire, amesema wilaya hiyo imejipanga vyema kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kutokana na taarifa za kutokea kwa baadhi ya wagonjwa wa "Marburg" kwenye mkoa wa Kagera ambao upo jirani zaidi na wilaya ya Chato.
Mganga mkuu wa wilaya ya Chato, Dk. Eugen Rutaisire,akizungumza na vyombo vya habariMbali na kuipongeza Wizara ya afya kwa kushirikiana na WHO kufika haraka wilayani humo kuimalisha kamati za majanga na dharula ili kuwa na uelewa wa pamoja na jamii,amesema elimu hiyo itawafikia wananchi walioko kwenye jamii ya chini zaidi ili watambue thamani ya kujilinda.
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa waganga wa tiba asili na tiba mbadala wilayani hapa, Pumuka Masanja,amewataka waganga wa jadi kujiepusha na kung'ang'ania wagonjwa ambao watagundua kuwa magonjwa yao huenda yanatokana na milipuko ili kunusuru maisha ya wagonjwa na familia zao, badala yake wawaelekeze haraka kwenda Zahanati,Vituo vya afya na hospitali kwaajili ya matibabu sahihi.
Post a Comment