HEADER AD

HEADER AD

AICT YAJIPANGA KUFANYA TAMASHA LA MUZIKI WA INJILI MKOANI SHINYANGA

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga

KAIMU Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Kanisa a Afrikan Inland Church Tanzania (AICT) Fabian Fanuel amefanya ziara ya kikazi katika Dayosisi ya Shinyanga ambapo amepata nafasi ya kufanya mazungumzo ya na Makamu Askofu Mkuu AICT ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga Zakayo Enock Bugota ofisini .

Mazungumzo hayo yamefanyika ofisi ya Askofu Mei, 16,2023, mazungumzo yamehusisha mambo kadha ya kiutendaji na kujitambulisha baada ya uteuzi wa nafasi hiyo pamoja na majadiliano ya kazi ambazo zinaendelea katika Dayosisi hiyo katika nyanja mbalimbali.
     Kulia ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Kanisa a Afrikan Inland Church Tanzania (AICT) Fabian Fanuel akiwa na Makamu Askofu Mkuu AICT ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga Zakayo Enock 

Kadhalika mazungumzo hayo yamejikita katika Maandalizi ya tamasha kubwa la muziki wa injili (Inland Festival 2023) katika Dayosisi ya Shinyanga na uwashwaji wa matangazo ya Inland Radio katika Mkoa wa Shinyanga.

Vilevile Fanuel amepata muda wa kukaa kikao cha kwanza na kamati ya maandalizi ya tamasha hilo ambalo kwa Dayosisi ya Shinyanga linategemea kufanya maeneo manne tofauti kama vile Bariadi, Maswa, Kahama na Shinyanga Mjini.

Kwa upande wa Askofu Bugota amepongeza kazi ambazo Idara ya Habari na Mawasiliano AICT imekuwa ikifanya katika kutekeleza majukumu na mikakati yake na kuiomba iendelee kufanya kazi kwa nguvu kuhakikisha wanafikia malengo tarajiwa.

No comments